Wednesday, 5 April 2017NA K-VIS BLOG, DODOMA
KATIBU wa Bunge, Dkt. Thomas Kashilila, ametangaza matokeo ya uchaguzi wa wabunge watakaoingia kwenye bunge la Afrika Mashariki, (EALA), huku wateule kutoka Chama Cha  Demokrasia na Manedeleo (CHADEMA), wakishindwa kupata kura za kutosha.
Akitangaza matokeo hayo mapema leo asubuhi Aprili 5, 2017 bungeni mjini Dodoma, Dkt. Kashilila aliwatangaza wabunge watano kutoka Chama Cha Mapinduzi CCM, na mbunge mmoja kutoka Chama Cha Wanachi (CUF) huku nafasi mbili zikiachwa wazi.
Walioshinda ni pamoja na Dkt. Gwaru Jumanne Maghembe, Alhaji Adam Kimbisa, Dkt.Abdul Makame, Mariam Ussi Yahya, Fancy Haji Nkuhi na Happiness Elias Mkigo wote kutoka CCM, wakati kutoka CUF, ni Mhandisi Habib Mnyaa.
Aidha Dkt. Kashilila alisema, wagombe wawili waliopendekezwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, hawakuchaguliwa kutokana na kupata idadi ndogo ya kura zilizowakubali na hivyo nafasi hizo mbili bado ziko wazi.
Akifafanua kuhusu matokeo hayo, Dkt. Kashilila alisema, Idadio ya wabunge kikatiba ni 394, walioshiriki ni 390, na waliopiga kura ni 334 na kura zilizoharibika ni moja.
Kundi A Wanawake, Fancy Haji Nkuhi kura 197, Happiness Elias Lukigo kura 196, Happiness Mgalula kura 125, na Zainab Rashid Kawawa kura 137.
Kwa upande wa kundi B Tanzania Zanzibar, Abdul Hasum Makame kura 254, Mohammed Yusuf Nuhu kura65, Maria Ussi Yahya kura 195 na Rabia Hamid Mohammed kura 242.
Upande wa kundi C vyama vya upinzani, walikuwa wagombea wawili, Ezekiel Dibogo Wenje kura za ndio 124 huku kura za hapana 174, Lawrence Kego Masha, kura za ndio 126 na kura za hapana 198 hivyo hakuna mshindi kwenye kundi hilo.
Kwa upande wa Chama Cha CUF, kundi C, wagombea walikuwa wanne, Habib Mohammed Mnyaa kura 188, Sonia Juma Magogo kura 6 Twaha Issa Taslima kura 140
Tanzania Bara kudni D, walioshiriki wagombea wane, Adam Omar Kimbisa 266, Anmringi Isaya Macha kura 23, Charles Makongoro Nyerere kura 81 na Gwaru Jumanne Maghembe kura 287
Ndg. Maryam Ussi YAHYA (CCM)

Ndg. Abdullah Hasnu MAKAME (CCM)

Wagombea wasimamizi wakijiandaa kwenda kuhesabu kura zao.

Dkt. Ngwaru Jumanne Magembe(CCM)

Happiness Elias Lugiko(CCM)
Fancy Haji NKUHI(CCM)

Habibu Mohamed MNYAA(CUF)Reactions:

0 comments:

Post a Comment