Sunday, 9 April 2017

Kikao cha Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kimekutana  leo Jumapili Aprili 9, 2017 na miongoni mwa maamuzi yake  kimeamua kuwa Mkutano Mkuu wa TFF, utafanyika Jumapili ya Agosti 12, 2017.
Taarifa ya TFF iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Aprili 9, 2017 imesema miongioni mwa ajenda katika mkutano huo, itakuwa ni uchaguzi mkuu wa TFF. Kwa mujibu wa Katiba, uchaguzi huo utachagua Rais wa TFF, Makamu Rais wa TFF na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment