Thursday, 13 April 2017

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) Prof Musa Assad akizungumza na waandishi wa Habari(hawapo Pichani) kuhusu Ripoti ya Ofisi yake kwa mwaka wa Fedha unaoisha 2015/2016 Leo Aprili 13,2017 Mjini Dodoma.Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) Prof. Musa Assad na Mwenyeketi Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe.Naghenjwa Kaboyoka  na Mbunge wa Sumbawanga mjini, Ayeshi Hilari, wakiangalia moja ya kitabu cha Ripoti kutoka Ofisi yake wakati alipokutana na  na waandishi wa Habari,(hawapo Pichani) kuhusu Ripoti ya Ofisi yake kwa mwaka wa Fedha unaoisha 2015/2016 Leo Aprili 13,2017 mjini Dodoma.(PICHA ZOTE NA RAYMOND MUSHUMBUSI MAELEZO DODOMA)


NA K-VIS BLOG, DODOMA
MKAGUZI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, (CAG), Profesa Mussa Assad,(pichani), amesema, Shirika la umeme Tanzania (TANESCO), haliwezi kupata faida kwa vile gharama za kununua umeem ni kubwa ukilinganisha na gharama za kuuza umeme huo kwa walaji.
Alisema TANESCO inanunua umeme kutoka kwa wazalishaji, Shilingi 545 kwa unit na kuuza kwa walaji (watumiaji), Shilingi 280 kwa unit moja.
“Kwa hiyo TANESCO inapata hasara ya Shilingi 265 kwa kila unit moja ya umeme inaouuza”. Alisema Profesa Assad.
Profesa Assad aliayasema hayo leo Aprili 13, 2017 wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma leo Aprili 13, 2017 mjini Dodoma wakati akiwasilisha ripoti yake ya ukaguzi ya mwaka 2015/2016.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment