Friday, 7 April 2017Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Rushwa Nchini, Valentino Mlowoka akitoa mada kwa washiriki wa semina ya wabunge pamoja na mada nyingine kujadili pia ufanisi wa vyombo vya Kupambana na Rushwa ndani ya Ukanda wa Afrika Mashariki kuhusu maswala ya rushwa, matokeo na madhara yake mjini Dodoma leo. Semina hiyo iliandaliwa na Mtandao wa Bunge wa Afrika Kupambana na Rushwa (APNAC), kushirikiana na Asasi ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Vijana Tanzania chini ya udhamini  wa Taasisi ya Kijamii ya Afrika. (Picha na Robert Okanda Blogspot)
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Rushwa Nchini, Valentino Mlowoka akiongea na washiriki wa semina ya wabunge wakati kutoa mada mbalimbali kwenye semina ya pamoja ya ufanisi wa vyombo vya Kupambana na Ruswa ndani ya Ukanda wa Afrika Mashariki kuhusu maswala ya rushwa, matokeo na madhara yake mjini Dodoma

Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson akiongea na washiriki wa semina ya wabunge iliyokuwepo na mada  mbalimbali ambapo walijadili ufanisi wa vyombo vya Kupambana na Ruswa ndani ya Ukanda wa Afrika Mashariki kuhusu maswala ya rushwa, matokeo na madhara yake mjini Dodoma leo. Semina hiyo iliandaliwa na Mtandao wa Bunge wa Afrika Kupambana na Rushwa (APNAC), kushirikiana na Asasi ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Vijana Tanzania chini ya udhamini  wa Taasisi ya Kijamii ya Afrika. Kutoka (kulia) ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Rushwa Nchini, Valentino Mlowoka, Katibu wa APNEC, Daniel Mtuka na Mwenyekiti wa APNEC, George Mkuchika

Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson akiteta jambo na Mwenyekiti wa APNEC, George Mkuchika.

Wabunge wakifuatilia mada kwa makini wakati waliposhiriki semina iliyojadili maswala ya kupambana na rushwa pamoja ya ufanisi wa vyombo vya Kupambana na Ruswa ndani ya Ukanda wa Afrika Mashariki kuhusu maswala ya rushwa, matokeo na madhara yake mjini Dodoma leo. Semina hiyo iliandaliwa na Mtandao wa Bunge wa Afrika Kupambana na Rushwa (APNAC), kushirikiana na Asasi ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Vijana Tanzania chini ya udhamini  wa Taasisi ya Kijamii ya Afrika.

Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki na watoa mada wa mkutano wa wabunge wakati wa semina hiyo leo. Kutoka (kulia) ni Mtafiti Moses Kulaba, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Rushwa Nchini, Valentino Mlowoka, Katibu wa APNEC, Daniel Mtuka na Mwenyekiti wa APNEC, George Mkuchika.

Mwenyekiti wa APNEC, George Mkuchika akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum, Dkt. Mary Mwanjelwa, Pia Mbunge wa Makete, Profesa Norman Sigalla baada ya kumalizika kwa semina hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Vijana Nchini Tanzania, Israel Ilunde.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment