Tuesday, 25 April 2017


Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kulia), akimkabidhi kitabu chenye sheria mbalimbali za Bunge la Tanzania, Mhe. Douglas Syakalima, (wa pili kushoto), ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya Miundombinu na Kiongozi wa Msafara kutoka Bunge hilo la Zambia, Wabunge hao wamekuja kubadilishana uzoefu na kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu katika kikao kilichofanyika leo Aprili 25, 2017,ukumbi wa Spika mjini Dodoma. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson na kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu Mhe. Profesa. Norman Sigala King.

 Picha ya pamoja

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na Waheshimiwa Wabunge kutoka Bunge la Zambia ambao pia ni Wajumbe wa kamati ya Miundombinu kutoka Bunge hilo waliokuja kubadilishana uzoefu na kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, katika kikao kilichofanyika leo Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Prof. Norman Sigala King akizungumza na Waheshimiwa Wabunge kutoka Bunge la Zambia ambao pia ni Wajumbe wa kamati ya Miundombinu kutoka Bunge hilo waliokuja kubadilishana uzoefu na kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, katika kikao kilichofanyika leo Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

Reactions:

0 comments:

Post a Comment