Sunday, 2 April 2017

Kiungo wa timu ya Simba James Kotei raia wa Ghana  ambaye anauwezo wa kucheza namba zaidi ya moja Uwanjani akipambana kupata mpira mbele ya wachezaji wa kagera Sugar leo hii uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Na Faustine Ruta, Bukoba
Timu ya soka ya Kagera Sugar imefanikiwa kuichapa timu ya Simba kwa bao 2-1 katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara, uliopigwa katika dimba la Kaitaba, Mjini Bukoba Mkoani Kagera.

katika mchezo huo ulishuhudia timu ya soka ya Simba wakishindwa kutumia nafasi zao vyema walizopata na kujikuta wakifungwa bao 2-1 ambapo mabao ya Kagera Sugar yalifungwa na Mbaraka Yusuph na bao la pili likifungwa na Edward Christopher huku bao la kufutia machozi kwa Simba likifungwa na Mzamilu Yasin dakika 61 ya kipindi cha pili. 

Kwa matokoe hayo Yanga wanaendelea kuwa kileleni mwa ligi hiyo wakiwa na jumla ya pointi 56 wakifuatiw na Simba wenye pointi 55 huku Kagera Sugar wakifikisha jumla ya pointi 45 huku nafasi ya nne ikishikwa na Azam wenye pointi 44.
Kikosi cha Simbakilicholala mbele ya Kagera Sugar kwenye ligi kuu soka Tanzania Bara mjini Bukoba Aprili 2, 2017
Kikosi cha Kagera Sugar "kilichoidhalilisha" Simba
Mshambuliaji wa timu ya Simba Mrundi Laudit Mavugo akijaribu kumtoka Beki wa Kagera Sugar Juma Ramadhan .
Shizah Ramadhan Kichuya Akiambaa na Mpira.
Kiungo wa timu ya Simba Said Ndemla akiachia Shuti kali ambalo lilipanguliwa na Kipa Juma Kaseja
Kiungo wa timu ya Simba James Kotei raia wa Ghana  ambaye anauwezo wa kucheza namba zaidi ya moja Uwanjani akipambana kupata mpira mbele ya wachezaji wa kagera Sugar leo hii uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Wachezaji wa Kagera Sugar wakishangilia moja ya magoli waliyofunga
Viongozi wa Simba, Mwenyekiti Nyange Kabouru, (kushoto), na Hans Pope(mwenye mpama)
Mohammed Ibrahim wa Simba (kulia), akikokota mpira mbele ya mlinzi wa Kagera Sugar
Mecky Mexime Kocha wa Kagera Sugar akiwa amebebwa na Wachezaji wa Kagera mara baada ya kuibuka na Ushindi wa bao 2-1.
Simba walipata bao lao la pekee kipindi cha pili dakika ya 61 na mtanange kuwa 2-1.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment