Monday, 3 April 2017LICHA ya kupoteza pointi tatu muhimu mbele ya Kagera Sugar kwenye pambano lililopigwa uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba Jumapili Aprili 2, 2017, baada ya kufugwa mabao 2-1 kwenye pambano la ligi kuu soka Tanzania Bara,wekundu wa Msimbazi,  Simba wamepokelewa kishujaa na mashabiki wa timu hiyo, wakati walipowasili mkoani Geita leo Aprili 3, 2017.
Simba itaweka kambi ya siku nne kujiandaa na mchezo dhidi ya Mbao FC na Toto Africans zote za Jijini Mwanza, michezo ambayo itapigwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwamza.

Ikiwa Mkoani Geita Simba inatarajia kucheza mchezo wa Kirafiki na timu ya Geita Gold Sport Siku ya Jumatano mechi ambayo itachezwa kwenye uwanja wa shule ya msingi  Waja.

Kwa Mujibu wa Nahodha wa Simba, Jonas Mkude, amewaomba mashabiki kuendelea kuiunga mkono timu yao na kwamba wataakikisha wanafanya vizuri kwenye
michezo  iliyombele yao
 (IMEANDALIWA NA JOEL MADUKA WA MADUKA ONLINE BLOG).

Reactions:

0 comments:

Post a Comment