Monday, 10 April 2017NA DAUDI MANONGI-MAELEZO, DODOMA.
SERIKALI kupitia Halmashauri zilizo katika maeneo ya migodi imeanza kuweka mikakati ya kudhibiti magonjwa ya Kifua kikuu na Silicosis kwa kutoa Elimu kwa wachimbaji  wa madini ikiwemo kujikinga na vumbi na kutumia njia sahihi za uchimbaji.
Hayo yamesemwa na Naibu Naibu WazirwAfya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Khamis Kingwangalla, (pichani) leo Aprili 10, 2017  Bungeni Mjini Dodoma wakati wa Maswali na Majibu.
“Tanzania inafahamu changamoto ya uwepo wa magonjwa  haya ya kifua kikuu na Silicosis katika maeneo ya wachimbaji, kwa upande wa Kifua kikuu tatizo hili ni kubwa lakini kuwekuwepo na ripoti za wagonjwa wachache wa Silicosis  katika hospitali za Serikali ikiwemo Kibong’oto”,Alibainisha Mhe.Kigwangalla.
Ameeleza kuwa kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na Magonjwa ya UKIMWI,Kifua Kikuu, na Malaria wa Global Fund to Fight AIDS,Tuberculosis na Malaria nchi kumi wananchama wa jumuiya ya SADC ikiwemo Tanzania ziko katika utekelezaji wa mpango wa kudhibiti kifua kikuu na magonjwa ya mfumo wa hewa yatokanayo na uchimbaji madini ikiwemo Silicosis.
Aidha katika mpango huo kuna afua  itakayo shughulika na sera  za udhibiti wa vumbi katika maeneo ya wachimbaji ambayo itawabana wachimbaji kudhibiti vumbi wakati wa shughuli za uchimbaji.
“Serikali itaongeza wigo wa huduma katika vituo vya afya kwenye maeneo yaliyoathirika ikiwemo Mkoa wa Geita ili vituo viwe na uwezo wa kuchunguza na kutibu magonjwa haya na kuwajengea uwezo wataalamu wa afya katika kuhudumia wagonjwa katika maeneo ya migodi”Alisisitiza Mhe. Kingwangalla.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment