Monday, 3 April 2017

TIMU ya taifa ya vijana ya Tanzania, Serengeti Boys, wameonyesha maajabu baada ya kusawazisha mabao 2 katika dakika 10 za mwisho wa mchezo wa kirafiki wa kimataifa wa kujipima nguvu dhidi ya timu ya soka ya taifa ya vijana ya Ghana kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo Aprili 3, 2017.
Ghana walianza kupata mabao yao mapema kupitia Sulley Ibrahim kabla ya Arko Mensah kuongeza la pili.
Hadi dakika za nyongezwa zinaonyeshwa, Serengeti ilikuwa nyuma kwa mabao mawili. 
Lakini dakika ya 90+5, mshambuliaji hatari wa Serengeti Boys, Assad Juma akafunga bao la mkwaju wa penalti baada ya beki wa Ghana kuunawa mpira eneo la hatari.
Dakika ya 90+10,  Muhsin Malima akavunja mtego wa kuotea na kumalizia kazi nzuri ya kiungo wao.
Bao hilo liliamisha shamrashamra uwanjani hapo na ikaonyesha kweli Boys wanastahili kuchangiwa, wanastahili kuandaliwa ili wakafanye vizuri nchini Gabon katika michuano ya Kombe la Mataifa Afrika.
Screen-Shot-2017-04-03-at-7.38.11-PM
Reactions:

0 comments:

Post a Comment