Tuesday, 4 April 2017

Profesa Kitila Alexander Mkumbo.
NA K-VIS BLOG
RAIS John Pombe Magufuli, amemteua Mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Profesa Kitila Mkumbo, kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji leo Aprili 4, 2017. Mbali na kazi yake hiyo ya Uhadhiri, pia
Profesa Kitila Alexander Mkumbo ni Mshauri wa masuala ya siasa wa chama cha upinzani ACT-Wazalendo, na kwenye orodha rasmi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyotolewa na Katibu wa Bunge hilo, Dkt. Thomas Kashilila, Aprili 3, 2017 Profesa Mkumbo ametajwa kuwa ni pendekezo la chama cha ACT Wazalendo kama mgombea wao wa uchaguzi wa wabunge wa bunge la Afrika Mashariki, (EALA) unaotarajiwa kufanyika baadaye leo jioni bungeni mjini Dodoma.

Profesa Mkumbo,  anachukua nafasi ya Mhandisi Mbogo Futakamba ambaye amestaafu. Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu iliyosambazwa kwa vyombo vya habari muda mfupi uliopita, Rais pia amemteua Dkt. Ave Maria Semakafu, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi, (MUHAS), kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Taarifa kamili ya Ikulu inapatikana hapachini ambayo inaonyesha wengine walioteuliwa.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment