Saturday, 1 April 2017Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wajumbe wa Kamati Maalum ya kuchunguza kiwango cha aina ya madini yaliyomo kwenye mchanga wenye madini ulio ndani ya makontena yaliyozuiliwa na Serikali sehemu mbalimbali hapa nchini mara baada ya kuwaapisha Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Aprili 1, 2017.(PICHA NA IKULU)


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Profesa Abdulkarim Hamis Mruma aliyekuwa akitoa neno la Shukrani mara baada ya wajumbe wote kuapa.

 Rais akimpongeza Mwenyekiti wa Kamati, Profesa Mruma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya kuchunguza kiwango cha aina ya madini yaliyomo kwenye mchanga wenye madini ulio ndani ya makontena yaliyozuiliwa na Serikali sehemu mbalimbali hapa nchini Profesa Abdulkarim Hamis Mruma Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha mmoja wa wajumbe wa Kamati hiyo Profesa Justinian Rwezaura Ikungula Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha mmoja wa wajumbe wa Kamati hiyo Profesa Joseph Buchweishaija Ikulu jijini Dar es Salaam
 Rais akizungumza na wana kamati baada ya kuwaapisha Ikulu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake, Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn wakati akijiandaa kupanda ndege kwenye  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kurejea nchini kwake mara bada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili jijini Dar es Salaam.


Vikundi mabalimbali vya ngoma pamoja na ushereheshaji vikishangilia wakati Rais Dkt. John Magufuli pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa walipokuwa wakizungumza kuhusu Serikali kuthamini mchango wa vikundi hivyo.

 Rais Magufuli, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wakizungumza na washereheshaji pamoja na vikundi mbalimbali vya ngoma  uwanjani hapo (JNIA). Wakwaza kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda
Reactions:

0 comments:

Post a Comment