Thursday, 20 April 2017


Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji Mhe. Charles Mwijage, (kulia), akiuliza jambo mbele ya  Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF, Bi. Janet Ezekiel na  Afisa Mfawidhi wa PPF, Bw. Astro Liganga wakati alipotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonesho ya Mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi, yanayoendelea kwenye viwanja vya Mashujaa mjini Dodoma, Aprili 21, 2017.


Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Kazi,Vijana, Ajira na Wenye ulemavu), Mhe.Anthony Peter Mavunde, (kulia), akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la PPF katika Maonesho ya Mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi  baada ya kupata maelezo ya mpango wa ‘ Wote scheme’ ambao umekua msaada katika kuwaongezea mitaji vijana kutokana na mikopo ya mpango huo. Kushoto ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF Bi.Janet Ezekiel na  Afisa Mfawidhi wa PPF Astro Liganga.


NA MWANDISHI WETU, DODOMA
MFUKO wa Pensheni wa PPF unaendelea kuwakumbusha wananchi kujiunga na Mfuko huo ili kuweza kufaidika na fursa mbalimbali kama vile mikopo ya maendeleo, elimu, huduma ya afya, mafao ya uzeeni na mafao ya uzazi.

Akiongea katika Maonesho ya uwezeshaji wananchi kiuchumi katika viwanja vya Mashujaa, mkoani Dodoma, Aprili 20, 2017, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF Bi.Janet Ezekiel alisema hii ni fursa pekee kwa waajiriwa wapya wakiwemo walimu, madaktari na kada zingine kuchagua Mfuko wa Pesheni wa PPF ili kuweza kukidhi mahitaji yao ya kimaendeleo.

Bi. Janet alisema waajiriwa hao wapya wakijiunga na PPF watafaidika na mikopo katika maeneo yao ya kazi, mafao ya uzazi, mafao elimu, mafao ya ugonjwa, mafao ya kifo, wategemezi, kiinua mgongo na mafao ya uzeeni yanayolipwa kwa wakati kwa kutumia kikotoo kilichoboreshwa.Afisa Mwendeshaji wa PPF, Kanda ya Mashariki na Kati Joyce Rwechungura akitoa maelezo ya kazi mbalimbali zinazofanywa na PPF kwa wananchi waliotembelea banda la PPF katika Maonesho ya Mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi yanayoendelea inayoendelea katika viwanja vya Mashujaa mkoni Dodoma.

Mbunge wa jimbo la Ushetu Mhe.  Elias Kwandikwa, (kulia) akiuliza swali juu  mpango wa ‘Wote scheme’ ulivyofanikiwa kwa watu wote ikiwemo walio kwenye Sekta isiyo rasmi nao kupata nafasi ya kupata mafao mbalimbali. Wanaomsikiliza kwa makini  ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF Janet Ezekiel na  Afisa Mfawidhi wa PPF Astro Liganga


Katibu wa Chama cha Wafugaji Tanzania Magembe Makoye akimsikiliza kwa makini Afisa Mfawidhi wa PPF Astro Liganga kuhusu Mfumo wa ‘Wote scheme’ ambao kima cha chini cha kuchangia ni shilingi elfu ishirini na ndani yake kuna fursa za mikopo ya maendeleo, mikopo ya elimu, huduma za afya na mafao  ya uzeeni. Mfumo huu unawawezesha wote walio katika sekta isiyo rasmi kujiwekea akiba.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment