Friday, 14 April 2017KAMISHINA wa Operesheni na Mafunzo wa jeshi la  polisi, Nsato Marijani, akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani, wakati akitoa tamko kuhusu operesheni itakayoendeshwa na jeshi hilo ya kuwasaka wahalifu waliohusika na mauaji ya Askari nane katika msitu wa Jaribu Mpakani Mkoa wa Pwani juzi. Kushoto ni Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba ''Tunaomba wananchi watusamehe kwa operesheni hii tunayokwenda kuianza, kwani askari wanane ni wengi sana na hatutakuwa na msalie mtume kwa hili, wameanza sisi tunamaliza, na jana ilikuwa ni 8 - 4, lakini tukianza nawaambia mabao yetu yatakuwa ni zaidi yao'';. alisema Marijani Aidha Marijani ametangaza kuwa eneo hilo ni marufuku waendesha pikipiki kupita zaidi ya saa kumi na moja jioni. Kaa nasi (KWA HISANI YA SUFIANI MAFOTO BLOG)

Reactions:

0 comments:

Post a Comment