Thursday, 13 April 2017NA K-VIS BLOG
HABARI za awali zinasema askari polisi wanaokadiriwa kuwa watano wameuawa katika shambulio la kuvizia wilayani Kibiti mkoa wa Pwani, Aprili 13, 2017.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, amethubitisha kutokea kwa tukio hilo lakini hakutaja idadi kamili ya askari polisi waliouawa.
“Ni kweli askari wetu wanaokadiriwa kuwa watano, wakiwa katika gari lao la doria, wakitoka eneo la Jaribu Mpakani kurejea Kibiti walishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana na gari lao likapinduka lakini bado sijapata idadi kamili ya waliouawa.” Alisema.
Waziri Nchemba alisema, kimsingi shambulio hilo wanalichukulia kama ni kulipiza kisasi kwa wahalifu hao dhidi ya askari polisi ambao wamekuwa wakifanya kazi nzuri ya kuwadhibiti wahalifu hao ambao kwa sasa wanatafuta mahala pa "kujificha" mkoani Pwani baada ya kufurushwa jijini Dar es Salaam.
Waziri amesikitishwa na shambulio hilo na kuwataka Watanzania kuwa watulivu wakati jeshi la polisi linaendelea na operesheni ya kuwasaka wahalifu hao ambapo aliongeza kuwa taarifa kamili ya tukio hilo baya, itatolewa na Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani leo Aprili 14, 2017.
Kumekuwa na matukio ya polisi na watumishi wa serikali kushambuliwa na wahalifu mkoani Pwani ambapo tukio la hivi karibuni kabisa, polisi walimuua mwanamume mmoja aliyejaribu kuwatoroka polisi akiwa amevalia vazi la hijab linalovaliwa na wanawake.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

Wakati huo huo taarifa za kipolisi kutoka mkoani zimethibitisha kuuawa kwa askari wake wanane,(8), eneo la Mkengeni, kijiji cha Uchembe Kata ya Mjawa, wilaya ya Kibiti mkoani Pwani, majira ya saa 12:15 jioni Aprili 13, 2017.
Taarifa ya polisi iliyotolewa leo Aprili 14, 2017 inasema kundi la majambazi ambalo idadi yao haijulikani wakiwa na silaha walilishambulia kwa risasi gari la polisi namba PT 3713 Toyota Land Cruiser na kuwauwa askari nane.
Taarifa hiyo ya polisi imewataja waliouawa ni pamoja na Inspekta Kigugu, Koplo Francis, Konstebo wa polisi Haruna, Konstebo wa polisi Jackson, Konstebo wa polisi Zacharia, Konstebo wa polisi Siwale, Konstebo wa polisi Maswi, na Konstebo wa polisi Ayoub.
Taarifa imesema, katika shambulizi hilo la kuvizia, askari mmoja Konstebo wa polisi Frederick, alijeruhiwa na risasi kwenye mkono wake wa kushoto na alikimbizwa kwenye hospitali ya Misheni ya Michukwi kwa matibabu.
Aidha taarifa inasema, baada ya kufanya mauaji hayo, walipora silaha tisa za askari hao ambazo ni aina ya SMG sita zikiwa na risasi 30 kila moja na long range tatu.
Taarifa hiyo ya polisi ilifafanua kuwa polsii hao walikuwa wakitoka kwenye kizuizi cha barabarani, (Road Block cha Jaribu Mpakani baada ya kubadilishana lindo na walikuwa wakielekea Bungu na gari lilipofika eneo la Mkenge ambapo kuna mteremko na majani, majambazi hayo yalilishambulia gari hilo upande wa mbele wa dereva  na hivyo kusababisha gari kupoteza mwelekeo na kutumbukia mtaroni na hivyo majambazi hao waliwashambulia kwa risasi.
Waziri Mwigulu Nchemba
 
Wakati huo huo taarifa za kipolisi kutoka mkoani zimethibitisha kuuawa kwa askari wake wanane,(8), eneo la Mkengeni, kijiji cha Uchembe Kata ya Mjawa, wilaya ya Kibiti mkoani Pwani, majira ya saa 12:15 jioni Aprili 13, 2017.
Taarifa ya polisi iliyotolewa leo Aprili 14, 2017 inasema kundi la majambazi ambalo idadi yao haijulikani wakiwa na silaha walilishambulia kwa risasi gari la polisi namba PT 3713 Toyota Land Cruiser na kuwauwa askari nane.
Taarifa hiyo ya polisi imewataja waliouawa ni pamoja na Inspekta Kigugu, Koplo Francis, Konstebo wa polisi Haruna, Konstebo wa polisi Jackson, Konstebo wa polisi Zacharia, Konstebo wa polisi Siwale, Konstebo wa polisi Maswi, na Konstebo wa polisi Ayoub.
Taarifa imesema, katika shambulizi hilo la kuvizia, askari mmoja Konstebo wa polisi Frederick, alijeruhiwa na risasi kwenye mkono wake wa kushoto na alikimbizwa kwenye hospitali ya Misheni ya Michukwi kwa matibabu.
Aidha taarifa inasema, baada ya kufanya mauaji hayo, walipora silaha tisa za askari hao ambazo ni aina ya SMG sita zikiwa na risasi 30 kila moja na long range tatu.
Taarifa hiyo ya polisi ilifafanua kuwa polsii hao walikuwa wakitoka kwenye kizuizi cha barabarani, (Road Block cha Jaribu Mpakani baada ya kubadilishana lindo na walikuwa wakielekea Bungu na gari lilipofika eneo la Mkenge ambapo kuna mteremko na majani, majambazi hayo yalilishambulia gari hilo upande wa mbele wa dereva  na hivyo kusababisha gari kupoteza mwelekeo na kutumbukia mtaroni na hivyo majambazi hao waliwashambulia kwa risasi
Reactions:

0 comments:

Post a Comment