Sunday, 23 April 2017NA K-VA BLOG NA MASHIRIKA YA HABARI

LILE pambano la watani wa jadi nchini Hispania, (El Clasico), baina ya Real Madrid na Barcelona la ligi kuu ya soka nchi humo maarufu kama Laliga, lilimalizika usiku wa kuamkia leo Aprili 24, 2017 kwa Barca kushinda mabao 3-2.
Hata hivyo Barca imeshinda Madridi ikiwa pungufu kufuatia mlinzi wake na nahodha wa timu hiyo, Sergio Ramos, kutolewa nje ka kadi nyekundu kufuatia rafu aliyomchezea mshambuliaji hatari wa Barca, Leonel Messi, zikiwa zimesalia si zaidi ya dakika 20 mpira kumalizika.
Pambano hilo lililokuwa la marudiano na kuchezwa kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu, Madrid ilikuwa ya kwanza kujipatia bao katika kipindi cha kwanza kupitia kwa kiungo wa kati wa timu hiyo Cacemiro, kufuatia mpira wa krosi uliopigwa na Marcello kutoka wingi ya kushoto.
Hata hivyo Barca ilisawazisha bao hilo dakika chache kabla ya mpira kwenda mapumziko kupitia kwa winga wake Ra
BAO la 500 la Lionel Messi limeipeleka Barcelona kwenye uongozi wa ligi kuu ya Hispania Laliga katika muda wa majeruhi dhidi ya wachezaji pungufu wa Real Madrid kwenye uwanja wa ugenini wa Santiago Bernabeu nchini Hispania usiku wa kuamkia leo Aprili 24, 2017
Ushindi wa mabao 3-2 wa el clasico dhidi ya hasimu wake Madrid, unaifanya Barca kuwa na pointi sawa na Madrid lakini kwa rekodi nzuri ya kukabana koo kileleni.
Casemiro alifunga bao la kwanza na la kuongoza kabla ya Messi kusawazisha na Ivan Rakitic kuiweka Barcelona mbele huku Nahodha wa Madrid, Sergio Ramos, al=kionyeshwa kadi nyekundu kutokana na kumchezea vibaya Messi.
Kocha Mkuu wa Madrid, Zenadine Zidane, “Zizu” alifanya mabadiliko kwa kumuingiza James Rodriguez ambaye alifunga bao la kusawazisha, kabla ya Messi kufunga bao la ushindi kwenye muda wa majeruhi.
Licha ya kufungwa katika pambano hilo, bado ina faida mchezo mmoja mkononi ukilinganisha na Barca ambayo sasa imesaliwa na michezo mitano.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment