Tuesday, 18 April 2017


Ndege ya kudondosha mabomu ya Russia, aina ya TU-95 Bear bombers, ambayo iliingiliwa safari zake na ndege vita mbili za Marekani aina ya F-22 Jumatatu Aprili 17, 2017

NA K-VIS BLOG/ MASHIRIKA YA HABARI
NDEGE vita mbili za kijeshi za Marekani zimeingilia kati mipango ya ndege ya kudondosha mabomu ya RUSSIA Jumatatu Aprili 17, 2018
Wizara ya ulinzi ya Marekani Pentagon imesema, ndege ya kudondosha mabomu ya Russia aina ya TU-95 Bear bombers, iliingiliwa mipango yake ya safari na ndege vita mbili za jeshi la Marekani aina ya F-22 Raptor kwenye anga la kimataifa pwani ya Alaska.
Uingiliaji huo wa safari ya ndege hiyo ya Ruassia, umeitwa na Pentagon kuwa ulikuwa wa kitaalamu na salama na ulitokea kiasi cha maili 100 kutoka kisiwa cha Kodiak ambapo ndege hiyo ya Russia ilijikuta ikiruka juu ya anga ya ukanda wa kiulinzi ya Alaska.
Hapakuwepo mawasiliano baina ya vyumba vya marubani wa ndege za pande mbili , maafisa wa Marekani wamesema.
Tukio hili linatokea wakati Marekani imekuwa katika vita vya maneno baina yake na mshirika mkuu wa Russia, Korea Kaskazini ambapo Marekani tayari imesogeza manowari yake ya kubeba ndege kwenye Rasi ya Korea huku Korea Kaskazini ikionye kuwa itajibiza kwa nguvu kubwa shambulio lolote la Marekani dhidi yake.

Ndege vita za Marekani aina kama hii F-22 zilitibua safari ya ndege vita ya kudondosha mabomu ya Ruassia aina ya TU-95 kwenye anga ya Alaska
Reactions:

0 comments:

Post a Comment