Saturday, 8 April 2017NA K-VIS BLOG
MBUNGE wa Mtama, Mhe. Nape Nnauye amemuomba Rais John Magufuli, kuunda tume kuchunguza vitendo alivyodai ni matumizi mabaya ya vyombo vya dola.
Akihutubia kwenye mkutano wa hadhara jimboni kwake leo Aprili 8, 2017, Nape alielezea jinsi yeye mwenyewe alivyotishiwa kwa bastola alipotaka kuzungumza na waandishi wa habari nje ya hoteli ya Protea karibu na Kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es Salaam.
Alisema, vitendo vya utekaji na utesaji ambavyo vinaonekana kushamiri nchini, ni ushahidi tosha wa Rais kuunda tume hiyo ili kutenganisha serikali na vitendo hivyo viovu.

“Tulisikia kijana mmoja wa CHADEMA, Ben Saanane, a mepotea miezi mingi sasa, mazimgira ya kupotea kwake hayajaeleweka vizuri, watu wamevamia kwenye kwenye Studio za Televisheni wakiwa na silaha, nani Yule, aliyepewa dhamana akabeba silaha na kuingia kwenye kituo cha radio, na kuvamia.” Alisema na kuongeza
“Juzi tumesikia pale Dar es Salaam, wamevamia studio watu wanne wamevamiwa na hatujui wako wapi, mmoja wao anaitwa Roma Mkatoliki, watu hao hawajulikani waliko, mh, mimi mtoto wa Kimakonde, nitasema kweli daima, nilikwenda CCM sio kwa sababu ya magwanda ya kijani nilikwenda CCM kwa vile CCM tunasema sema kweli daima.”
“Matendo haya yanamjengea chuki yeye Rais na wananchi, itaonekana yeye ndiye anayewatuma, sasa ili kumuondolea chuki, ni vema aunde tume ili ichunguze na kumpatia majibu.”
Alisema pia, ili Mwenyekiti wangu wa CCM,  aitenganishe CCM na matendo ya wahuni wachache wanaotumia dhamana waliyopewa kuumiza watu na kupoteza watu.” Alisema.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment