Friday, 21 April 2017

NA MWANDISHI MAALUM
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Aprili 21, 2017, Dimond alisema  ameamua kuingia kwenye soko la kutengeneza pafyum zenye nembo yake CHIBU ili kusaidia serikali katika suala zima la kutatua changamoto ya uhaba wa ajira nchini.
Ameongeza kwamba kuanza kutengenezwa na kuuzwa kwa pafyum hizo kutaongeza ajira kwa vijana wengi lakini pia kutasaidia kukuza uchumi wa nchi kupitia kodi zitakazotozwa kutokana na bidhaa hiyo ambayo wanaume na wanawake wote wanaweza kuitumia, Pafyum ya CHIBU itapatikana katika maduka yote ya GSM na itauzwa bei ya rejareja kiasi cha shilingi 105.000 kwa moja.
Katika mkakati mwingine wa soko Meneja wa Msanii huyo Bw. Salaam Mendes amesema wako katika mazungumzo na mashirika kadhaa likiwemo shirika la ndege la Kenya Airways kwa ajili ya kuitangaza bidhaa hiyo na kuifikisha kwenye soko la kimataifa ikiwa ni pamoja na kuuzwa katika maduka makubwa kwenye viwanja vya ndege katika nchi mbalimbali ambako ndege za shirika hilo zinafika
17
Mwanamuziki Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Plutnamz akimkabidhi chupa ya Pafyum iitwayo "Chibu", Aisha Azori mteja wake wa kwanza aliyenunua bidhaa hiyo kwenye maduka ya GSM Mall jijini Dae salaam leo Aprili 21, 2017.
11
Mwanamuziki Naseeb Abdul maarufu, Diamond Plutnamz akizungumza na waandishi wa habari wakati akizindua Pafyum hiyo kulia ni Mmoja wa Mameneja wake Babu Tale.
1415
Meneja wa Diamond Plutnamz,  Salaam Medes akizungumza mara baada ya kuzindua pafyum hiyo kwenye duka kubwa la GSM Mall barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam.
16
Diamond akiionyesha pafyum hiyo
18
Bw. Salaam Mendes akitaja bei ya pafyum hiyo kwa waandishi wa habari mara baada ya kuizindua rasmi leo jijini Dar es salaam.Reactions:

0 comments:

Post a Comment