Wednesday, 5 April 2017
NA K-VIS BLOG
TAASISI ya Tiba ya Mifupa (MOI), leo Aprili 5, 2017 imepata Mkurugezni Mtendaji mpya, ambaye ni Dkt. Respicious Lwezimula Boniface.
Taarifa ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ILIYOSAINIWA NA Msemaji wa wizara hiyo, Bw.Nsachris Mwamaja, imesema, Waziri wa wizara hiyo, Bi. Ummy Mwalimu, amemteua Dkt. Boniface kuziba nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, ambayo ilikuwa wazi tangu mwaka 2014, baada ya aliyekuwa Mkurugenzi  Mtendaji kustaafu kwa mujibu wa sheria.
Nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, ilikuwa ikikaimiwa na Dkt.Othman Kiloloma.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment