Thursday, 6 April 2017

 Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhe. Alexander Mnyeti(kulia), akiongozwa na afisa wa bunge kuingia kwenye chumba cha mahojiano na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge baada ya kuitikia wito wa kamati hiyo, Bungeni mjini Dodoma leo Aprili 7, 2017. Mnyeti anatakiwa kujibu tuhuma zinazomkabili za kuingilia Haki, Uhuru na Madaraka ya Bunge kutokana na matamshi aliyoyatoa mapema mwaka huu Wilayani Arumeru Mkoani Arusha yaliyokuwa na madai ya kulidharau Bunge.(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhe. Alexander Mnyeti akihojiwa mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge baada ya kuitikia wito wa kamati hiyo, Bungeni mjini Dodoma leo, kujibu tuhuma zinazomkabili za kuingilia Haki, Uhuru na Madaraka ya Bunge kutokana na Matamshi aliyoyatoa mapema mwaka huu Wilayani Arumeru Mkoani Arusha yaliyokuwa na madai ya kuidharau Bunge.(PICHA NA OFISI YA BUNGE)


Reactions:

0 comments:

Post a Comment