Monday, 24 April 2017JEN1
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo, akiongozana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Uratibu, Ajira na Wenye ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama wakikagua maandalizi ya mwisho mwisho ya maadhimisho ya Sherehe za Miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwenye uwanja ya Jamhuri  mjini Dodoma. Maadhimisho hayo yataongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Jumatano Aprili 26, 2017.
JEN2
Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikiwa kwenye gwaride la maandalizi ya maadhimisho ya  miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika terehe 26 Aprili Mjini Dodoma.
JEN3
Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikiwa kwenye gwaride la maandalizi ya maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika terehe 26 Aprili Mjini Dodoma.
JEN4
Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikiwa kwenye gwaride la maandalizi ya maadhimisho ya  miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika terehe 26 Aprili Mjini Dodoma.
Askari wa Pikikipi maalum wakionesha namna pikipiki hizo zitakavyopamba maonesho hayo.
JEN6
Makomandoo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),wakionesha umahiri wao wa kuvuta gari lenye tani 7 ikiwa ni moja ya mbinu ya medan.
JEN7
Askari wa Kikosi cha Farasi wakionesha umahiri wao katika kutumia farasi kupambana na uhalifu.
JEN8
Wanafunzi wa halaiki wakipita kwa ukakamavu mbele ya Jukwaa Kuu.
NA IMMACULATE MAKILIKA- MAELEZO – DODOMA
MKUU wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo, na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu, Ajira na Wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama wametembelea uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma ili kujiridhisha na maandalizi ya sherehe za miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hapo Jumatano Aprili 26, 2015
Akizungumza baada ya kutembelea maandalizi hayo, Mhe. Mhagama ametoa rai kwa  Watanzania kuwa wazalendo pamoja na kudumisha amani na utulivu uliopo nchini. 
Akizungumza, leo mjini Dodoma wakati akifuatatilia maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano yatakayofanyika Aprili 26 mwaka huu katika Uwanja wa Jamhuri uliopo mjini Dodoma. 
“Tunapoadhimisha miaka 53 ya Muungano ninawaomba watanzania kuwa wazalendo pamoja na kulinda amani ya nchi” alisema Waziri Mhagama Pia, Waziri Mhagama aliwaomba watanzania hasa wakazi wa Dodoma kuhudhuria kwa wingi katika Maadhimisho hayo yatakayofanyika jumatano wiki hii. Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alisema kuwa mkoa wake umejipanga vizuri katika kufanikisha maadhimisho hayo, ambapo pia alivishukuru vyombo vya habari kwa kuhamasisha wananchi juu ya maadhimisho hayo. 
“Wananchi wamehamasika kushiriki katika maadhimisho haya ya miaka 53 ya Muungano, ninawashukuru kwa kazi kubwa mliyoifanya na tunaamini mtaendelea kuhamasisha wananchi kushiriki katika maadhimisho hayo” alisema Rugimbana Maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano yamehudhuriwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Christina Mndeme, pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali. 
Aidha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, ambapo pia yatahudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein na viongozi mbalimbali wa dini na  Serikali. Maadhimisho hayo ya miaka 53 ya Muungano yanatarajiwa kupambwa namaonesho kutoka  kutoka vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama, burudani za  vikundi vya ngoma pamoja na maonesho ya halaiki.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment