Wednesday, 5 April 2017

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi mashine ya kufulia nguo Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua Mwalimu Ali Simai Makame, kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Wazee wa Viongozi wa Wilaya ya Mkoani Pemba wakati alipowasili katika majengo ya Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua Mkanyageni kuzungumza na wanafunzi wa skuli hiyo wa kuwapatia vifaa kwa ajili ya matumizi yao. ya kila siku skulini hapo.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akiwasili katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba.
Wananchi wa Wilaya ya Mkoani Kisiwani Pemba wakimpokea Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, alipowasili katika Ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua Mkoani Pemba.
Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua wakiimbi wimbo wa Sisi Sote Tumekomboka wakati wa hafla ya kukabidhiwa Vifaa mbalimbali na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, alipofika Skulini hapo.
Mwanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua  Ali Shariff akisoma Quran kabla ya kuaza kwa hafla hiyo. 
Mwalimu Mkuu wac Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua Ali Simai Makame akitowa maelezo ya Skuli hiyo wakati wa hafla hiyo ya Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, kukabidhi misaada mbalimbali kwa Wanafunzi wa Skuli hiyo.
Mkurugenzi Idara wa Idara Sekondari Bi. Idrisa akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi misaada kwa wanafunzi wa Skuli hiyo mpya ya Sekondari Wilayani Mkoani Pemba. 
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman akitowa nasaha zake kwa Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua Wilaya ya Mkoani Pemba wakati wa hafla hiyo.
Mjumbe wa Umoja wa Wake wa Wawakilishi na Wabunge Bi Asha Shamsi akisalimia na kutowa nasaha zake kwa Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua Wilaya ya Mkoani Pemba.
Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Pemba Mhe Hemed Suleiman akijibu maswali yaliowakilishwa wakati wa hafla hiyo na Uongozi wa Skuli ya Sekondari kwa kupata uhaba wa Maji. na kuwalazimu wanafunzi kufuata maji katika maeneo ya nje ya skuli yao. 
Naibu Waziri Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mmanga Mjengo Mjawiri pia ni Mwakilishi wa Jimbo las Mkanyageni akizungumza wakati wa hafla hiyo na kumkaribisha Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, kuzungumza na Wanafunzi wa Skuli hiyo. 
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwahutubia na kutowa nasaha zake kwa Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua alipofika kuwatembelea na kuwakabidhi vifaa kwa ajili ya matumizi yao ya kila siku skulini hapo.
Wanafunzi wa Kidatu cha Kwanza katika Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, wakati alipofika kuwatembelea na kuwakabidhi misaada kwa ajili ya matumizi yao skulini hapo. 
Wanafunzi wa Kidatu cha Kwanza katika Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, wakati alipofika kuwatembelea na kuwakabidhi misaada kwa ajili ya matumizi yao skulini hapo. 
Mwalimu wa Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua, Subira Othman Hafidh akitowa neno la shukrani kwa Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, na Ujumbe wake wa Wake wa Wawakilishi na Wabunge wa CCM kwa msaada wao na umewafikia wakati muafaka.
Mwananchi wa Kijiji cha Mkanyageni akisoma dua baada ya kumalizika kwa hafla hiyo ya kukabidhi vifaa kwa Wanafunzi wa Skuli hiyo.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi mashine ya kufulia nguo Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua Mwalimu Ali Simai Makame, kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi sabuni Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua Mwalimu Ali Simai Makame, kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman.na kulia Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Mmanga Mjengo Mjawiri.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi risiti ya vifaa hivyo Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua Mwalimu Ali Simai Makame, kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman.na kulia Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Mmanga Mjengo Mjawiri.


Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua Wilaya ya Mkoani Pemba. baada ya kumaliza hafla ya kukabidhi vifaa kwa wanafunzi wa Skuli hiyo.
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blog
Zanzinews.com.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment