Sunday, 23 April 2017Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar  Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein akimpongeza Mbunge wa Jimbo la Mfenesini  Kanali (mstaafu), Masoud Khamis, wakati wa hafla ya kukabidhi magari manane (8), aina ya Dyna  yenye thamani ya shilingi milioni 192, yaliyotolewa na mbunge huyo kwa CCM ili kusaidia shughuli za chama visiwani Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar  Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Gari Nane(8) ya CCM aina ya Dyna ikiwa ni ahadi ya Mbunge wa  CCM wa Jimbo la Mfenesini Col.Mstaafu Masoud Khamis (wa pili kulia) katika viwanja vya Z. Ocean  Hotel iliyopo kihinani Wilaya ya Magharibi Jimbo la Mfenesini


Magari manane (8) aina ya Dyna  yaliyonunuliwa na Mbunge wa Jimbo la Mfenesini, kisiwani Unguja,  Kanali (mstaafu), Masoud Khamis ambazo leo amezikabidhi kwa Chama cha Mapinduzi CCM zitakazotumika na kutoa huduma katika Matawi ya CCM katika jimbo hilo. Magari hayo yaliyopokelewa na Makamu Mwenyekiti wa CCM, (Zanzibar), Rais wa Dkt. Ali Mohammed Shein, zimegharimu shilingi Milioni 100 na tisini na mbili. (PICHA NA IKULU ZANZIBAR)
Reactions:

0 comments:

Post a Comment