Saturday, 8 April 2017Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, (KUB), na Mbunge wa Hai, (CHADEMA), Mhe. Freeman Mbowe, na Mbunge wa Kawe, (CHADEMA), Mhe. Halima Mdee kwa nyakati tofauti , leo Aprili 8, 2017 wamefikishwa mbele ya Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kufuatia amri ya Mhe. Spika wa Bunge Job Ndugai ya kuwataka wafike mbele ya kamati hiyo kujibu tuhuma zinazowakabili za kuingilia Haki, Uhuru na Madaraka ya Bunge kutokana na matashi yao. Pichani Mhe. Mbowe, akiingia kwenye chumba cha mahojiano. picha za chini, zinaonyesha Mhe. Mbowe na Mhe. Mdee wakiwa mbele ya Kamati kwa nyakati tofauti. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)
Reactions:

0 comments:

Post a Comment