Wednesday, 26 April 2017

wapinga kombora la kujihami la Marekani THAAD

NA K-VIS BLOG NA MASHIRIKA YA HABARI
CHINA imezidi kuukoleza mgogoro wa Rasi ya Korea baina ya Marekani na Korea Kaskazini kwa kuzindua meli yake kubwa ya kubeba ndege Aprili 26, 2017.
Ni meli ya pili ya kubeba ndege baada ya ile ya Liaoning na ya kwanza iliyotengenezwa ndani ya nchi.
Meli hiyo ambayo bado haijapewa jina, ilipelekwa kwenye bandari ya Kaskazini Mashariki ya Dalian, Shirika la Habari la Serikali limesema. Meli hiyo itaanza kufanya kazi mnamo mwaka 2020.
Wakati China ikifanya hivyo Korea Kaskazini, ilifanya mazoezi yake ya kijeshi kwa ambapo ilirusha maroketi kutoka kwenye vifaru vilivyojipanga kandokando ya bahari.
Kwa upande wake mamia ya wananchi wa Korea Kusini, waliandamana jana kupinga kuwasili kwa makombora ya kujihami ya Marekani yajulikanayo kama Terminal High-Altitude Area Defense (THAAD).na kamanda wa vikosi vya Marekani vilivyoko bahari ya Pacific, Admirali Harry Harris amesema, Marekani itakuwa tayari katika teknolojia yake bora kabiosa kudhibiti tishio lolote la makombora kutoka Korea Kaskazini.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment