Friday, 7 April 2017MAREKANI imerusha makombora 59 aina ya Tomahawk cruise missiles, dhidi ya ngome za kijeshi za Syria usiku wa kuamkia leo Aprili 7, 2017.
Taarifa za vyombo vya habari zinasema, tayari mshirika mkuu wa Syria, Russia, imeomba kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kiitishwe ili kujadili mashambulizi hayo.
Marekani inasema mashambulizi hayo ni kujibiza matumizi ya silaha za kemikali ambazo Syria ilizitumia hivi karibuni dhidi ya wapinzani wake na kuua watu wapatao 100., Hata hivyo Syria imekanusha kutumia silaha za kemikali, “sumu”.
Serikali ya Syria inasema mashambulizi hayo ya usiku kucha yamepelekea raia sita kuuawa madai ambayo yamekanushwa vikali na Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon), ambayo imesema mashambulizi hayo hayakuwalenga raia isipokuwa yalilenga ngome za kijeshi, jimbo la Magharibi la Homs.
Makombora hayo yalirushwa kutoka kwenye meli ya kivita ya Marekani, USS Ross na USS Porter zilizotia nanga kwenye bahari ya Mediterranean na kuelekzwa kwenye ngome za Shayrat, ambayo Marekani inadai, ngome hiyo ndiyo iliyotumika kuanzisha mashambulizi ya anga Jumanne iliyopita yaliyokuwa na silaha za kemikali na kupelekea vifo vya watu 100.
Mashambulizi hayo yameibua hasira kali kutoka Russia ambayo imekuwa ikiiunga mkono Syria katika vita hiyo ya kikabila iliyodumu kwa miaka 6 sasa
Moscow imesema utawala wa Assad haujawahi kutumia silaha za sumu (kemikali) na kwamba Marekani imetumia shambulio la Jumanne iliyopita kama sababu
 


Reactions:

0 comments:

Post a Comment