Wednesday, 19 April 2017


1
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akiongoza maandamano ya wasanii wa Bongo Movie kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa huyo kwenda Kariakoo jijini Dar es Salaam leo Aprili 19, 2017, ambako mkutano mkubwa umefanyika  ukiwa na lengo la kuzindua kampeni kabambe ya kupambana na mawakala wa kuchapisha na kuuza filamu za nje ya nchi zinazoingizwa kinyume na utaratibu na sheria huku zikiwa hazilipiwi kodi, Jambo ambalo linafifisha biashara ya filamu za wasanii wa Tanzania kutokana na kuuzwa kwa bei ya chini ukilinganisha na filamu za nyumbani ambazo zinalipiwa kila kodi kwa mujibu wa sheria
Makonda amewatahadharisha watu wote wanaoingiza filamu  kutoka nje ya nchi bila kulipa kodi  huku wakijua kwamba hawana mikataba ya kusambaza au kuuza kazi za wasanii hao , amewataka wauzaji wadogo wadogo kujiunga vikundi na kusajiliwa ili wapewe vitambulisho ili watambulike wakati wanafanya kazi za kuuza kazi hizo za sanaa zikiwemo filamu na nyimbo.
235
Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie wakiimba nyimbo za kumshangilia Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Bw. Paul Makonda wakati wakiwa kwenye maandamano kuelekea Kariakoo ambako kumefanyika mkutano mkubwa wa uzinduzi wa kampeni ya kuzuia uuzaji wa kaza za filamu bila kufuata utaratibu na sheria za nchi.
6
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaa  Paul Makonda akiwasili katika eneo la mkutano.
78
Baadhi ya wasanii  pamoja na wananchi wakiwa katika mkutano huo.
  10
Waigizaji Kajala, Masanja na Dokii wakiwa katika mkutano huo.
11
Katibu Tawala wa mkoa wa Dar es salaam Theresia Mmbando akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuhutubia.
12
Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie wakiwa katika mkutano huo.
13
Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie na wananchi wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika mkutano huo.
15
Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh Sophia Mjema akizungua  katika mkutano huo.
16
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda katikati akimsikiliza Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi. Bi. Joyce Fissoo wakati akizungumza katika mkutano huo.
17
Kamanda Wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamishna Simon Sirro akizungumza katika mkutano huo ambapo ameonya wale wote wanaouza filamu za Ngono na za kigaidi amesema hao watapambana na mkono wa dola.
18

19
Reactions:

0 comments:

Post a Comment