Thursday, 20 April 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, (wkwanza kushoto), akiweka jiwe la msingi kuzinduaujenzi wa mradi wa umeme wa gesi wa Kinyerezi II, jijini Dar es Salaam, Machi 16, 2016.(PICHA YA MAKTABA)


NA K-VIS BLOG
SERIKALI kupitia Shirika lake la Umeme Nchini, (TANESCO), litaokoa kiasi cha Dola bilioni moja kila mwaka zitokanazo na kununua mafuta ya kuendesha mitamboya kufua umeme, baada ya kukamilika kwa miradi ya uejnzi wa mitambo ya kufua umeme wa gesi ya Kinyerezi II, III na IV.
Tayari mradi wa Kinyerezi II wenye thamani ya Dola za Kimarekani Bilioni 432 ambao ni sawa na asilimia 15% ya miradi inayokusudiwa kuanza, umeshazinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Machi 16, 2016.
Kwa ujumla wake, mradi wa usambazaji mabomba ya kusafirisha gesi utakamilika mnamo mwaka 2022 ambapo karibu vinu vyote vya gesi vuitakuwa vimekamilika, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini, (TPDC), Bw. Kapuulya Musomba, ameviambia vyombo vya habari wiki hii.
Imeelezwa kuwa Mabomba ya kusafirisha gesi toka Mtwara-Dar es Salaam na vinuvya kuchakata gesi pale Madimba navisiwa vya Songosongo vinafanya mipango ya serikali kuongeza umeme wa Megawati 2,000, (2,000MW), kutoka mashine mpya za kufua umeme wa gesi mwakani, 2017, na hivyo kuiongeza uwezo wa kuzalisha umeme hadi kufikia Megawati 10,000 (10,000MW), ifikapo mwaka 2025.
Hata hivyo ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya hivi majuzi, Profesa Mussa Assad, imeibua vikwazo Fulani kuhusiana na ugunduzi mpya wa mafuta na gesi ambapo alisema kwa sasa mabomba ya kusafirisha gesi yanatumika chini ya kiwango kutokana na kuchelewa kwa ujenzi wa mitambo ya kufua umeme wa gsi pale Kinyerezi.
KaimuMkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Bw. Musomba. Kwa upande wake anasema, mabomba ya kusafirisha gesi imepangwa yaweze kukamilika katika kiwango chake cha juu kwenye kipindi cha miaka 10.
Machi 23, 2017, Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), liliiomba Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ishauri Serikali kuruhusu mizigo(mitambo), yake iliyokaa bandarini kwa muda mrefu kutokana na swala la kodi iruhusiwe ili iweze kukamilisha ujenzi wa Mradi wa Umeme wa Gesi wa Kinyerezi I&II.
TANESCO ilitoa ombi hilo wakati wa ziara ya Kamati hiyo iliyofanya kwenye Mradi huo jijini Dar es Salaam, Machi 23, 2017 ili kujionea maendeleo ya ujenzi wa Mradi huo  muhimu.
“Mashine na vifaa vilivyozuiwa bandarini viruhusiwe ili vikakamilishe mradi wa umeme wa Kinyerezi I&II na kodi zinazopaswa kulipia mashine hizo zilipwe baadaye ili kuruhusu kazi ya kufunga mitambo hiyo kwenye Mradi huo iweze kukamilika kwa wakati.” Alisema Meneja wa Mradi kutoka TANESCO akiiambia kamati hiyo
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka, naye aliongeza  kwa kusema, “inatupa shida wakati mwingine, fedha zinatakiwa zilipwe kule bandarini, uwezo wa TANESCO katoka makusanyo sio mzuri sana kutokana na madeni, hivyo kama tungeweza kuruhusiwa kutoa vifaa hivyo bandarini, ingekuwa vema kwani kasi ya ukusanyaji mapato ya TANESCO inapoongezeka ndivyo tunavyoweza kulipa lakini Mradi utakuwa umeendelea.” Alisema Dkt. Mwinuka.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment