Friday, 7 April 2017

NA K-VIS BLOG
WIZARA ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, imetoa rai kwa wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kutoa taarifa zitakazosaidia kupatikana kwa mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Ibrahim Mussa, maarufu kama Roma Mkatoliki ambaye yeye pamoja na wenzake watatu, Moni na Bello na Emma“walitekwa nyara” Aprili 5, 2017 wakiwa kwenye studio ya Tongwe jijini Dar es Salaam.
Taarifa ya wizara iliyosainiwa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Bi. Zawadi Msalla, ilisema, “Wizara imepokea kwa mshtuko taarifa za kutoweka kwa mwanamuziki Ibrahim Mussa kwa jina la kisanii.” Ilisema taarifa hiyo.
Taarifa hiyo ilisema wizara inafuatilia kwa karibu swala hilo kwakuwa lina muelekeo wa kijinai ingawa taarifa kutoka vyombo vya dola zinathibitisha kuwa Roma Mkatoliki hashikiliwi kwenye kituo chochote cha polisi.
Kamanda Simon Sirro
 KAMANDA wa polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP, Simon Sirro, amethibitisha kupokea taarifa za “kutekwa” kwa msanii Ibrahim Mussa maarufu kama Roma Mkatoliki.
Kamanda Sirro hata hivyo ameonya watu waache kukimbilia kuilaumu serikali kutokana na tukio hili, “Tusi-conclude kuwa serikali inahusika, tukio hili ni kama matukio mengine, Ufuatiliaji unafanyika, inawezekana ni watu wabaya wamefanya hivyo, tunajaribu kufuatiilia kama kuna mambo ya ugoni au nini, ni vema watu wakatulia wakati polisi inaendelea kuchunguza.” Alisema.
Naye mke wa Roma, Nancy aliwaambia waandishi wa habari kuwa yeye alipokea simu majira ya saa 7 usiku wa Aprili 6 akipewa taarifa za kupotea kwa mumewe na kwamba anaiomba vyombo vya sheria na serikali kusaidia mumewe apatikane.
Roma na mkewe Nancy
Kwa upande wake mmiliki wa studio ya Tongwe Records mahala ambako tukio hilo la “kutekwa” kwa roman a wenzake lilifanyika, Jay Mart, alisema, watu watano wakiwa kwenye gari aina ya NOAH, walifika kwenye studio yake na kuulizia kama nipo, walipoambiwa kuwa sipo, walimuhitaji Roma, na kufaya mahojiano naye pamoja na vijana wengine waliokuwepo, kasha wakachukua TV, Camera na Kompyuta na kuondoka navyo pamoja na akina Roma
Reactions:

0 comments:

Post a Comment