Saturday, 22 April 2017NA K-VIS BLOG NA MASHIRIKA YA HABARI
Gareth Bale kucheza Jumapili
Isco
MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Real Madrid, Gareth Bale huenda akawemo kwenye kikosi chake kitakachomenyana na Barcelona katika pambano la watani wa jadi “El Clasico” la marudiano la ligi kuu ya soka nchini humo maarufu kama “Laliga”.
Gareth Bale
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kutoka Wales, ameshindwa kucheza mechi 2 zilziopita kutokana na maumivu ya misuli lakini ameonekana kwenye mazoezi ya kikosi chake Alhamisi iliyopita.
Isco na Mbwa wake aliyempachika jina Messi
Barcelona watamkosa mshambuliaji wake wa kimataifa kitoka Brazil, Neymar ambaye anatumikia adhabu baada ya kutolewa nje kwenye mchezo wa timu yake dhidi ya Malaga Aprili 8.Madrid ambayo ina mchezo mmoja mkononi inaongoza ligi hiyo ikifuatiwa na Batcelona kwa tofauti ya pointi tatu.
El clasico mashabiki huchukiana wazi wazi:Mc Manaman
Mchezaji wa zamani wa Real Madrid, akihojiwa na BBC-Radio 5 kuhusu mchezo huo alisema, “El Clasico" sio kama vile pambano la Everton na Liverpool, au hata Liverpool na Manchester United, hapa tunazungmzia ushabiki uliokubuhu. Mashabiki kwenye El Clasico huchukiana timu hizi zinapokutana, nilikuwepo pale wakati nachezea Madrid, ambapo Luis Figo alirushiwa kichwa cha Nguruwe na shabiki”, anasimulia Mc Manaman.
“Palikuwa na askari wenye silaha wakimlinda kocha mkuu, huku mitutu ikiwa imeelekezwa kwa watu. Kama ingekuwa Uingereza hayumkini ungeshtushwa na hali hiyo. Na kwa vyovyote vile pambano hili huleta msisimko wa hali ya juu miongoni mwa washabiki.” Alisema.
Ni wakati wa Isco kung’aa
YAWEZEKANA ana unazi na Barcelona, akimiliki mbwa mdogo aliyempa jina la Messi na wakati wa majira ya joto wiki chache zilizopita, alihusishwa kuwa na mpango wa kujiunga na vijana wa Nou Camp, lakini sasa Francisco Roman Alarcon Suarez maarufu kwa jina la Isco anaweza kuwa na jukumu kubwa la kuipatia Real Madrid faida kubwa kwenye mbio zake za kuwani kombe la La Liga, dhidi ya Barcelona katika El Clasico pale Bernabeu.
Real Madrid inaingia mchezoni ikiwa mbele kwa pointi 3 dhidi ya hasimu wake Barcelona na mchezo mmoja mkononi.
Ushindi kwenye mechi hiyo ya Jumapili utaiwezesha Madrid kuwa na pointi sita mbele ya mpinzani wake, ambaye atakuwa na michezo mitano (5) iliyosalia.,
Swali ni je Isco ambaye hujulikana kama kijana wa ajabu (Wonder boy), yuko tayari kuweka mizania miongoni mwa nyota wa Galaxy hapo Bernabeu?
Kihistoria nyota ya kiungo huyo mshambuliaji, Isco ilianza kung’ara wakati akiichezea Valencia kwa mara ya kwanza mwaka 2010 akiwa na umri wa miaka 18, na alizidi kupata umaarufu baada ya kuhamia timu yake ya nyumbani Malaga wakati wa majira ya joto mnamo mwaka 2011.
Akiwa na vijana walioanza kung’ara pamoja akina Javier Saviola, Joaquin and Roque Santa Cruz, alikuwa muhimu wakati Malaga ikiongozwa na Manuel Pellegrini, iliingia kwenye fainali ya ligi ya mabingwa ya msimu wa 2012/13 ambapo ilifika hadi robo fainali kabla ya kutolewa na kwa kichapo cha mabao 2-0 wakati wa muda wa majeruhi dhidi ya Borussia Dortmund ya Ujerumani.
Kiwango cha Isco kwenye mashindano hayo kilipelekea kupewa tuzo ya kijana wa dhahabu (Golden Boy), kwa mchezaji bora kijana barani Ulaya, lakini pia aling’ara kwenye mashindano ya kimataifa akiwa na timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 21 mwaka 2013 ambapo Hispania iliibuka bingwa.
Ilikuwa wazi kuwa ubora wake usingemuwezesha kuendelea kuchezea Malaga kwani wakati wa majira ya joto, 2013 Real Madrid na kusajiliwa kwa kitita cha Euro Milioni 23 kwa mkataba wa miaka mitano.Reactions:

0 comments:

Post a Comment