Saturday, 8 April 2017KATIBU Tawala wa wilaya ya Kigamboni Ndg Rahel Mhando, leo tarehe 8/4/2017 amefungua mkutano wa baraza la wafanya biashara wa wilaya ya Temeke na Kigamboni.
Mhando amewataka wafanya biashara kuendelea kushirikiana na serikali katika kufanya biashara zao na kwamba kwa upande wa serikali wanaendelea kuchukua hatua mbalimbali kuboresha mazingira ya kufanya biashara na kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji.
Amewasihi wafanya biashara hao kuendelea kuzingatia sheria za nchi na matakwa ya serikali ikiwemo kulipa kodi zote za serikali zinazotakiwa kulipwa kutokana na biashara wanazofanya.
Mhando pia amewakaribisha wafanyabiashara na wawekezaji katika wilaya mpya ya Kigamboni kwani ni sehemu yenye fursa mbalimbali za kibiashara na uwekezaji.
"......Kigamboni ni wilaya mpya na ina fursa nyingi za kibiashara na uwekezaji, karibuni huku, msing'ang'anie kubanana katika maeneo mengine wakati Kigamboni kuna fursa za waziwazi..., karibuni sana..... " Amesisitiza Rahel Mhando.Reactions:

0 comments:

Post a Comment