Wednesday, 19 April 2017NA K-VIS BLOG, DODOMA
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameamua kuwa, Madaktari 258 ambao waliokuwa tayari kwenda kufanya kazi nchini Kenya waajiriwe na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara moja.
Kwa mujibu wa taarifa ya Waziri wa Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu, aliyotoa leo Aprili 19, 2017 mjini Dodoma
Imesema uamuzi huo unafuatiwa kutofuatwa kwa mkataba baina ya serikali ya Kenya na Tanzania, uliosema utekelezaji wa ajira hizo za Madaktari ilikubalika na pande zote mbili kuwa iwe imekamilika ifikapo tarehe 6 Aprili, 2017 na kuwa  Madaktari hao wawe tayari kusafiri kwenda nchini Kenya kati ya tarehe 6-10 Aprili, 2017 tayari kuanza kazi.
Hata hivyo taarifa hiyo imesema, wananchi (Madaktari) watano wa Kenya waliwasilisha pingamizi Mahakamani kuitaka Serikali ya nchi yao kusitisha kuajiri Madaktari kutoka Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Mhe. Waziri Ummy, Madaktari waliokubaliana mapema na tangazo hilo la serikali, majina ya Madaktari husika na vituo watakavyopangiwa kazi yatatangazwa katika tovuti ya Wizara www.ehealth.go.tz pamoja na wataalamu wengine wa Afya 11 walioleta maombi yao na kukidhi vigezo.
Aidha, Serikali ya Tanzania itakuwa tayari kushughulikia upya ombi la Serikali ya Kenya kupatiwa Madaktari 500, pale ambapo hakutakuwa na vikwazo vya kupeleka Madaktari wetu nchini Kenya, taarifa ya Waziri imesema.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment