Tuesday, 4 April 2017

 Rais mstaafu wa awamuya nne Dkt. Jakaya Kikwete, mwanaye Ally Kikwete, (kushoto), na msaidizi wake, wakiimba wimbo wa taifa kwenye sehemu ya wageni wa Spika ndani ya ukumbi wa bunge mjini Dodoma leo Aprili 4, 2017 ambapo Bungelilizizima wakati Dkt. Kikwete akitambulishwa na Spika Mhe. Job Ndugai. Dkt. Kikwete alikuwa bungeni kumsindikiza mkewe Mama Salma Kikwete ambaye ameapishwa kuwa mbunge
 Rais Mstaafu Jakaya Kikwete aliposimama wakati wa utambulisho huo Bungeni leo.


  Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa na tabasam maridhawa wakati wa utambulisho huo Bungeni leo. Kushoto ni mwanaye Ally Kikwete pamoja na msaidizi wake
 Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa na tabasam maridhawa wakati wa utambulisho huo Bungeni leo. Kushoto ni mwanaye Ally Kikwete pamoja na msaidizi wake
Wabunge wakishangilia
 Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na mkewe, Mama Salma Kikwete, mara baada ya mamaSalma kuapishwa kuwa mbunge bungeni mjini Dodoma leo Aprili 4, 2017
  Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na mkewe, Mama Salma Kikwete na mtoto wao, Bw. Ally Kikwete.
Dkt. Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Mbunge wa viti maalum (CHADEMA), Dkt. Elly Macha

Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete, (katikati), akiwa na Katibuwa Bunge Dkt. Thomas Kashilila, (kushoto), na Katibu Mnyeka wa Spika wa Bunge, Bw.Said O. Yakubu, kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma leo Aprili 4, 2017. Dkt. Kikwete akiwa na familia yake, alifika bungeni hapo kumsindikiza mkewe Mama Salma Kikwete ambaye alikuwa anakula kiapo cha kuwa mbunge baada ya kuteuliwa na Rais, Dkt. John Magufuli. NA K-VIS BLOG, DODOMA

RAIS Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo Aprili 4, 2017 amelifanya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililoanza vikao vyake  mjini Dodoma "kutikisika" baada ya nderemo, vifijo kulipuka baada ya Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai, aliposimama kumtambulisha kwa wabunge.
Vifijo na shamra shamra hizo pia zilimshangaza Spikamwenyerwe ambaye alisema, "

“Hiki ni kipindi changu cha nne bungeni sijawahi kuona mgeni akipokewa namna hii” Alishangaa Mhe. Ndugai
Kupitia matangazo ya moja kwa moja ya runinga kutoka Bungeni mjini Dodoma, Mhe. Ndugai alisema "tuna mgeni maalum hapa Bungeni nae si mwingine ni Rais mstaafu Mhe. Jakaya Kikwete"
Baada ya utambulisho huo ndipo vifijo vilipolipuka toka kwa wabunge wote wa CCM na upinzani ambapo wengine walisikika wakisema “tumeku-miss sana na tunakukumbuka.” Dkt. Kikwete akiwa na baadhi ya watoto wake, alimsindikiza mama Salma ambaye ameapishwa leo kuwa mbunge kufuatia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kumteua kuwa mbunge hivi karibuni. 

Pamoja na kumsindikiza mkewe mama Slma, Rais mstaafu pia alipata fursa ya kusaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Mbunge wa Viti Maalum, (CHADEMA), marehemu Dkt.Elly Macha, hapo hapo kwenye majengoya bunge.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment