Sunday, 23 April 2017

SERENGETI-BOYS-1
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeandaa hafla maalumu ya kuchangisha fedha kwa ajili ya timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, Serengeti Boys Ijumaa ijayo.
Taarifa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, (TFF) imesema Serengeti Boys imeweka kambi nchini Morocco kujiandaa na fainali hizo zitakazoanza Mei 14 hadi 28, 2017 nchini Gabon.
TFF inatambua kuwa wadau mbalimbali wamekuwa wakichangia timu hiyo kupitia mitandao ya simu kama vile namba 0687 333 222 kadhalika Selcom kwa namba 22 33 44 pia kuweka fedha kwenye akaunti Na. 00 866 280 03 katika Benki ya Diamond Trust (DTB).
"Sasa siku ya Ijumaa Aprili 28, 2017 TFF imeandaa hafla maalumu ya kupokea michango hiyo, lakini pia kuchangisha fedha zaidi maana lengo ni kukusanya shilingi bilioni moja. Hafla hiyo itafanyika kwenye Hoteli ya Serena, Dar es Salaam kuanzia saa moja jioni."Taarifa hiyo imesema
TFF imeamua kutumia fursa kuwakaribisha wawakilishi wa makundi mbalimbali ili wawasilishe michango yao na kumkabidhi mgeni rasmi.
Kwa kutambua michango mbalimbali ambayo imekusanywa kupitia makundi ya mitandao ya jamii kama WhattsApp, facebook hivyo TFF inaomba wawakilishi wa makundi yote ya mitandao ya jamii (admins) ambao wamekusanya michango hii wajiorodheshe ili wapate fursa ya kukabidhi michango ya makundi yao kwa mgeni rasmi katika hafla hii.
Admins hawa wanaombwa wajiorodheshe kwa kutuma email kwenda fdf@tff.or.tz, kwa kupiga simu 0787 176767 au kwa kutuma ujumbe mfupi kwenda 0787 176767 ambayo pia inapatikana kwenye mawasiliano ya WhattsApp.
Aidha wawakilishi wa makundi mengine kama idara za Serikali, mashirika ya umma na binafsi kadhalika watu binafsi ambao nao wamechangia nao pia tunaomba wajioredheshe ili wapewe fursa pia ya kukabidhi michango yao siku hiyo ya Ijumaa.
TFF inashukuru sana kwa ushirikiano.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu ibariki Serengeti Boys
Reactions:

0 comments:

Post a Comment