Wednesday, 26 April 2017
NA K-VIS BLOG NA MASHIRIKA YA HABARI
ZAIDI ya akina mama 100,000 hupoteza maisha kila mwaka duniani kutokana na kuvuja damu nyingi baada ya kujifungua.
Kiasi cha asilimia 6% ya wanawake hupatwa na tatizo la kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua (postpartum hemorrhaging-PPH).
Na mara nyingi kukosekana kwa huduma za msingi za afya na madawa ndio huamua kati ya uhai na kifo kwa akina mama.
Lakini kuna ushahidi kuwa endapo kutakuwepo na gharama ndogo za madawa kunaweza kuokoa maisha wa akina mama watatu  kati ya hao.
Majaribio yanayohusisha wanawake 20,000 katika hospitali 193 kutoka nchi 21 hususan Afrika na Asia yamebaini kuwa upatikanaji wa dawa ijulikanayo kama tranexamic acid (TXA) kunaweza kuokoa maisha ya akina mama kwa asilimia 30 ya wanawake 100,000 wanaopoteza maisha duniani kutokana na kuvuja damu nyingi wakati wa kujifungua.
Katika kipindi cha masaa matatu baada ya kujifungua, mwanamke anayekuwa na tatizo la kuvija damu nyingi (PPH), walipewa TXA na ilionyesha kuwa wanawake wote waliopewa dawa hiyo iliwasaidia kuzuia kuvuja kwa damu na walipona.
"Kwa sasa tunao ushahidi muhimu kuwa matumizi ya mapema ya tranexamic acid (TXA), kunaweza kuokoa maisha ya mwanamke baada ya kujifungua na kutoa hakikisho la motto kukua na mama yake,” alisema Haleema Sakur kutoka shule ya masuala ya afya ya usai na madawa ya kitropiki ya jijini London ambayo ndiyo iliyoratibu jarinio hilo.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment