Sunday, 23 April 2017NA MWANDISHI WETU
FAINALI ya kwanza ya kombe la ligi Azam Sports Federation Cup, ambayo hutoa mwakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika,  itazikutanisha Simba na Azam FC katika nusu fainali ya kwanza itakayopigwa Aprili 24, 2017, kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Dro iliyochezeshwa Mubashara na kituo cha Televisheni cha Azam, jioni hii Aprili 23, 2017, Simba ndiyo itakuwa mwenyeji.
Kwa mujibu wa matokeo ya Droo hiyo, Yanga itakuwa mgeni wa Mbao FC katika nusu fainali ya pili itakayochezwa Aprili 30, 2017 jijini Mwanza.
Droo hiyo iliongozwa na Jemedari Said, Afisa Maendeleo ya TFF na Baruani Muhuza, Meenja wa Michezo wa Azam TV.
Aidha wawakilishi wa vilabu waliohudhuria Droo hiyo ni pamoja na, Said Tuly Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Simba, Meneja wa timu ya Azam, Naselida Zefania, Mjumbe wa Mbao FC na Hafidh ambaye ni Menenja wa Yanga.
Aliyekoroga vitufe vyenye majina ya timu alikuwa mchezaji wa zamani wa timu ya taifa, Iddi Moshi.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment