Wednesday, 26 April 2017


Na Shamimu Nyaki-WHUSM.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe ameliagiza Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kusimamia mashindano ya Miss Tanzania kwa ufanisi na kuhakikisha yanazingatia kanuni za uandaaji wa mashindano ya urembo.
Mhe. Mwakyembe ameyasema hayo jana Mjini Dododma   wakati alipokutana na Kamati ya Miss Tanzania iliyoongozwa na mwenyekiti, Hashim Lundenga  na kuwataka kusimamia vyema shindano hilo ili kupata washindi wenye viwango vinavyotakiwa Kimataifa.
“Nawaagiza BASATA simamieni shindano hili ili tupate washindi wenye viwango watakaosaidia Tanzania kujitangaza Kimataifa katika urembo”, Alisema Mhe. Mwakyembe.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Braza la Sana la Taifa (BASATA), Godfrey Muingereza amemuahidi Mhe Waziri Mwakyembe kuwa atasisamia kwa karibu na kwa ufanisi  mashindano ya Miss Tanzania ili yawe na ubora zaidi utakaowezesha nchi kufanya vizuri kwenye mashindano ya Dunia.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga ameahidi kushirikiana na Wizara pamoja na BASATA katika kuandaa na kuboresha   shindano la Miss Tanzania   ili kuwa na nguvu ya pamoja katika kupata ushindi utakaoletea Taifa heshima.
Mashindano ya Miss Tanzania yanayotarajiwa kufanyika baadae mwaka huu yanaandaliwa na kusimamiwa na Kamati inayoongozwa na Mwenyekiti, Hashim Lundenga, Katibu wake, Bosco Majaliwa na Mjumbe, Deo Kapten.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Miss Tanzania mara baada ya kufanya mazungumzo ofisini kwake Mjini Dodoma jana. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa, Godfrey Muingereza na Mwasisi wa Mashindano hayo, pia Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga (wa pili kushoto).  
Reactions:

0 comments:

Post a Comment