Wednesday, 19 April 2017NA K-VIS BLOG NA MASHIRIKA YA HABARI
BUNGE la Uingereza limepiga kura ya kuunga mkono pendekezo la Waziri Mkuu wan chi hiyo, Bi. Theresa May la kutaka Uingereza kufanya uchaguzi wa mapema Juni 8, 2017.
Theluthi tatu ya wabunge kama sheria inavyotaka walipiga kura ya ndio leo Aprili 19, 2017 na kukubaliana na pendekezo hilo ambalo Bi. May alisema juzi, kuwa uchaguzi mkuu wa mapema ndio utakaoleta mustakbala wa kitaifa.
Wananchi wa Uingereza walipiga kura ya kujitoa kwenye Jumuiya ya Ulaya na ili kutekeleza uamuzi huo wa wananchi ni shurti bunge liidhinishe kwanza.
Hata hivyo kumekuwepo na mgawanyiko mkubwa ndani ya bunge hilo hali inayotishia utengamano wa kitaifa.
Bi. May alisema, Waingereza ni wamoja lakini wabunge wan chi hiyo wamegawanyika na hivyo njia pekee ni kuitisha uchaguzi wa mapema nje na ratiba rasmi inayotaka uchaguzi mkuu wan chi hiyo kufanyika mwaka 2020

Reactions:

0 comments:

Post a Comment