Monday, 3 April 2017

 Mji wa pili kwa ukubwa nchini Russia, St. Petersburg

NA K-VIS BLOG/Mashirika ya habari-St.Petersburg
WATU 10 wameuawa kufuatia milipuko miwili kwenye kituo cha treni cha chini ya ardhi,(Underground), kwenye mji wa pili kwa ukubwa nchini Russia,  St.Petersburge.
Shirika la habari la serikali ya Russia, linasema, mlipuko mmoja umetokea kwenye kituo cha reli cha Senny Ploschad na kujeruhi watu 50.
Rais wa Russia, Vladimir Putin ambaye alikuwa kwenye mji huo kuhudhuria mkutano wa kiuchumi amearifiwa juu ya tukio hilo, shirika hilo la habari RIA, limeripoti leo Aprili 3, 2017 likimkariri msemaji wa Ikulu ya Russia, Kremlin.
Televisheni ya Al Jazeera, imesema mamlaka za mji huo zimefunga eneo lote linalozunguka vituo hicyo vya treni kama tahadhari ya mashambulizi zaidi.
Kikosi cha kupambana na ugaidi nchini humo kimethibitisha kutokea kwa milipuko hiyo.
Taarifa zaidi zinasema, bado haijafahamika kama milipuko hiyo ni vitendo vya kigaidi au la.Reactions:

0 comments:

Post a Comment