Thursday, 2 March 2017


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu You qing mara baada ya kuweka jiwe la Msingi katika Kiwanda kikubwa cha kutengeneza Vigae(Tiles ) cha Good Will kilichopo katika kijiji cha Mkiwa, Mkuranga mkoani Pwani. Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha vigae laki nane kwa siku na mwekezaji ametumia zaidi ya Dola mil.50 katika uwekezaji huo.(PICHA NA IKULU)


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Ikwiriri mkoani Pwani wakati alipokuwa akielekea mkoani Lindi na Mtwara katika ziara yake ya kikazi ya siku nne.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akihutubia kabla ya kuweka jiwe la Msingi katika Kiwanda kikubwa cha kutengeneza Vigae(Tiles ) cha Good Will kilichopo katika kijiji cha Mkiwa, Mkuranga mkoani Pwani.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwakilishi wa Kiwanda hicho cha  vigae cha Good Will, Huang Heng Chao  kutoka kwa Kiwandani hapo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipatiwa maelezo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kuhusu matumizi ya Gesi katika Kiwanda cha Vigae cha Good Will kutoka kwa Kiwandani hapo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mbunge wa Kilwa Kusini Suleiman Bungara, (Bwege ) kutoka CUF katika eneo la Nangurukuru, Kilwa mkoani Lindi wakati akiwa katika ziara ya mikoa ya kusini.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa  Nangurukuru  mkoani Lindi.


Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Nape Nnauye akifurahia hotuba iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika eneo la Nangurukuru mkoani Lindi.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Nape Nnauye mara baada ya kuhutubia wananchi wa Nangurukuru mkoani Lindi.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimian na mbunge wa Kilwa Kaskazini Vedasto Ngombale (CUF) mara baada ya kuhutubia wananchi wa Nangurukuru mkoani Lindi.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wananchi mara baada ya kuhutubia wananchi wa Nangurukuru mkoani Lindi.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpatia msaada wa Shilingi milioni moja kijana Abdulrahman Khalid ambaye ni mlemavu wa miguu katika eneo la Mchinga-1 mkoani Lindi, Katikati(Mwenye shati la maua) ni Mbunge wa Mchinga Hamidu Bobali kupitia chama cha (CUF) ambaye ameahidi kumpatia mlemavu huyo kiasi cha Shilingi Milioni moja pia.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment