Thursday, 23 March 2017


 na2
KWA wale watakaokumbuka vita ya Iraqi na Marekani, alikuwepo Waziri wa Habari wa serikali ya Sadam Hussein aliyejipatia umaarufu kutokana na taarifa zake kwa waandishi kuhusu hali ya vita hiyo ilivyokuwa ikipiganwa.
Waziri huyo aliitwa Mohammed El-Sahaf, ambaye licha ya mashambulizi makali yaliyokuwa yakitekelezwa na ndege za kivita za Marekani, dhidi ya majeshi ya Iraqi, lakini yeye alisimama kidete na kusema majeshi ya Iraqi yako imara na kuwaonya wanajeshi wa Marekani wasijaribu kuvuka "Faluja" na hapo watakiona cha mtema kuni.
Wamarekani walipoona anazidisha ngebe, wakashambulia jengo la ofisi yake aliyojuwa akitumia kufanya mikutano na waandishi wa habari.
Hata baada ya jengo hilo kuharibiwa vibaya na mashambulizi yakipamba moto, El-Sahaf alionekana akizungumza na waandishi wa habari mtaani. Leo hii Machi 23, 2017 ingawa haikuwa vita kama hiyo ya Iraqi,   aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alilazimika kuhutubia mkutano na waandishi wa habari akiwa "mtaani" tena juu ya gari lake,(kama anavyoonekana pichani),  baada ya uongozi wa Hoteli ya Protea iliyo jirani na Kanisa la Mtakatibu Petro, Oysterbay jijini Dar es Salaam, kukataa kumpa nafasi ya kufanya mkutano huo  kwa maagizo ya polisi.
Habari zinasema,Mhe. Nape ambaye ni Mbunge wa Mchinga (CCM), alituma ujumbe wa Twiter akisema atafanya mkutano na waandishi wa habari kwenye hoteli hiyo majira ya mchana, lakini alipowasili na gari lake kwenye eneo hilo, na kuteremka, polisi waliovaa kiraia walimvamia na kumuamuru arudi kwenye gari lake huku mmoja akimuonyesha bastola.
Hata hivyo Nape aliwasihi askari hao ambao walikuwa wanamsukuma kupunguza matumizi ya nguvu na kuwataka wasifanye hivyo. Wakati askari hao wakimlazimisha kurudi kwenye gari lake, kundi la waandishi wa habari liliingilia kati na kuwazuia askari hao kumsukuma Mhe. Nape na hapo ndipo alipoingia na kuhutubia mkutano huo akiwa juu ya gari lake.
Nape ambaye hadi kufikia jana Machi 22, 2017 alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Mkichezo, aliondolewa kwenye nafasi hiyo kwa kuteuliwa Dkt. Harrison Mwakyembe kushika wadhifa huo, katika mabadiliko madogo ya baraza la Mawaziri yaliyotangazwa leo jijini Dar es Salaam.
na3
na1

Baadhi ya maaskari wakiwa wameimarisha ulinzi katika eneo hilo.
na4
Reactions:

0 comments:

Post a Comment