Thursday, 2 March 2017SHIRIKA la Umeme Tanzania, (TANESCO), linawataarifu baadhi ya wateja wake wanaotumia huduma ya LUKU na kupata tabu kununu umeme kupitia baadhi ya mitandao ya simu za mikononi, (simu) hususan kipindi cha jioni kuanzia saa 11 mpaka saa 3 usiku.
Tatizo hilo linajitokeza kutokana na msongamano mkubwa wa wateja wanaokuwa wakinunua umeme katika muda huo uliotajwa hapo juu. Tayari Shirika linachukua hatua za haraka kwa kushirikiana na  wataalamu wa mitandao husika ili wateja waendelee kununua umeme wa LUKU kwa njia hiyo waendelee kupata huduma hiyo bila ya usumbufu wowote.
Wakati Shirika likiwa ninaendelea kushughulikia tatizo hilo, wateja wanashauriwa kununua umeme nyakati za Asubuhi na mchana ili kuepuka msongamano mkubwa kwenye mitandao hiyo ya simu lakini pia wateja wanaposhindwa kupata huduma wupitia mtandao fulani wanashauriwa kutumia mtandao mwingine wa simu.
Uongozi wa Shirika unaomba radhi kwa usumbufu wowote ule unaojitokeza kwa wateja.
IMETOLEWA NA OFISI YA:
MAWASILIANO NA MAHUSIANO TANESCO-MAKAO MAKUU
Reactions:

0 comments:

Post a Comment