Sunday, 19 March 2017


SHIRIKA la Umeme Tanzania TANESCO linawataarifu wateja wake wa maeneo ya Kimara, Mbezi yote na Kibamba yote kuwa, Kumetokea hitilafu katika Laini inayosambaza umeme katika maeneo hayo(NORDIC 1 &2) tangu jana Tarehe 18/03/2017 majira ya saa nane mchana Kutokana na Mvua kubwa iliyonyesha na kuathiri miundombinu ya umeme katika maeneo hayo na hivyo kupelekea kukosekana kwa huduma ya umeme kwa wateja wa maeneo hayo.
HATUA ZILIZOCHUKULIWA
Mafundi walichukua hatua za haraka kurejesha umeme tangu jana na kufanikiwa kurejesha huduma katika maeneo machache. Ili kurahisisha Kazi ya kubaini Hitilafu hiyo, Mafundi walilazimika kuzima laini zote mbili tena kwa siku ya leo na mpaka Hivi sasa mafundi wetu bado wako mtaani wakiendelea na jitihada za kurejesha umeme katika hali ya kawaida kwa maeneo yote yanayohudumiwa na laini hizi mapema iwezekanavyo.
Uongozi wa Shirika unaomba radhi kwa usumbufu wowote ule unaojitokeza.
Imetolewa na:
OFISI YA UHUSIANO TANESCO MAKAO MAKUU


Reactions:

0 comments:

Post a Comment