Wednesday, 1 March 2017

 Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi
wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii, nchini, (SSRA), Bi. Sarah Kibonde Msika, (kulia), akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandisi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam, Machi 1, 2017. Kushoto ni Afisa Mwandamizi wa TEHAMA wa Mamlaka hiyo, Bw. David Nghambi

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MAMLAKA ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii, nchini, (SSRA), imeanzisha mfumo wa TEHAMA, unaowezesha Wanachama wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini kutuma na kufuatilia malalamiko yao kwa urahisi.
Akielezea mfumo huo mbele ya Waandishi wa Habari leo Machi 1, 2017 kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO, jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa SSRA, Bi. Sara Kibonde Msika, amesema Mfumo huo unaiwezesha Mamlaka hiyo kupokea moja kwa moja.
Akifafanua zaidi, Afisa Mwandamizi wa TEHAMA wa Mamlaka hiyo, Bw.David Nghambi, amesema, Wanachama wanaweza “kupakua” (download), Mobile Application (App), unaopatikana kwenye simu za mikononi za Android kupitia Google play.
“Mfumo huu unatambuliwa kwa jina la SSRA, hivyo Mwanachama au Mwananchi yeyote baada ya kupakua App hiyo anaweza kutuma malalamiko yake kwa Mamlaka.” Alifafanua Bw. Nghambi.
Aidha Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa SSRA, Bi. Sara Kibonde Msika, alisema, Mamlaka imeanzisha Mfumo huo katika kutekeleza jukumu la kulinda na kutetea maslahi ya Wanachama wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. “SSRA iliyoanzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii, Sura ya 135(Toleo la 2015).” Alisema.
Alisema Mfumo huu unafaida nyingi kubwa zaidi umezingatia uwekaji mzuri wa kumbukumbu kwa upande wa Mamlaka na kurahisisha ufuatiliaji wa Mamlaka. Mfumo huu hutoa taarifa kwa upande wa Mamlaka na kurashisisha ufuatiliaji wa malalamiko.
“Mfumo huu hutoa taarifa za malalamiko ya Mwananchama kulingana na aina ya malalamiko, idadi na hatua ya utekelezaji iliyofikiwa, vilevile mfumo huu hutoa mrejesho kwa haraka kwa mlalamikaji bila kujali mahala alipo, hivyo mfumo huu ni rahisi kutumia na si lazima kwa Mwanachama kufika katika ofisi za Mamlaka.” Alisema Afisa mwandamizi wa TEHAMA wa SSRA, Bw.David Nghambi.
 Bw.David Nghambi. (Katikati), Bi. Sarah Kibonde Msika, (kulia), na Afisa wa TEHAMA wa SSRA, Bw.Ernest Masaka
 Bw.David Nghambi
 Baadhi ya waandishi waliohudhuria hafla hiyo wakiwa kazini
  Baadhi ya waandishi waliohudhuria hafla hiyo wakiwa kazini
 Mkutano ukiendeleaReactions:

0 comments:

Post a Comment