Sunday, 19 March 2017


NA K-VIS BLOG
MKURUGENZI wa uzalishaji vipindi wa kampuni ya Clouds Media Group, (CMG), Ruge Muitahaba, amethibitisha kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa na askari wenye silaha, amevamia ofisi za Clouds Ijumaa saa 10:45 usiku.
“Majira ya saa 10:45 napigiwa simu na Kitoi, kuna Crisis ofisini mlinzi amenipigia simu kuwa Mkuu wa Mkoa ameingia pale ofisini akiwa na askari 6 wenye silaha.
Hata hivyo Ruge akizungumza kwenye kipindi cha asubuhi cha 360 kinachopeperushwa na runinga ya Clouds, leo Machi 20, 2017, alsiema “Kwanza mimi nashangaa sana, nyinyi hamna hata diplomasia, mmeuliza moja kwa moja, nafikiri turudi nyuma kidogo lakini tunachozungumzia weekend hii kuanzia Alhamisi asubuhi. Tulikuwa na kipindi cha TCRA wakatupiga msasa, hapa hapa ofisini, katikati ya mkutano akaingia Mkuu wa Mkoa, tukasalimiana mara akapotea, niliposhuka nikamkuta Mkuu wa Mkoa akiwa na vijana wale wa SHILAWADU, wamemzunguka, nikawaona lakini nikawaacha, wakati ninataka kupanda gari langu,kijana mmoja akanijia na kuniambia Bosi tumepata tip hapa, kuna mama mmoja kazaa na Mchungaji Gwajima, lakini wakaniambia kuwa wamemtafuta Gwajima hawajampata, mimi nikawaambia kama hawajampata achaneni na hiyo story.”
“Alhamisi saa 10, nikapigiwa simu na mchungaji Gwajima, kwamba kuna vijana wako wa SHILAWADU kuwa wanakipindi kinachonihusu nikamwambia mimi sijui lakini nitafuatilia.”
“Nikawaambia hiyo story hata kwenye social media isitoke, kama hamjabalance story, na nikawaambia wale vijana, kama ule mkutano wenu mliokuwa ane pale Mkuu wa Mkoa juu ya kipindi hicho, basi muambieni kipindi hakitatoka.” Alisema Ruge.
Ijumaa tulikuwa busy, lakini nilitoa msisitizo kwa Kerry, kwamba waambie watu wako wa SHILAWADU, kile kipindi kisiruke, na nikamwambia Kitoi, HR, kuwa hicho kipindi kisitoke. Na ndani ya wenyewe wale SHILAWADU, palikuwa na mvutano baina yaoNilipokata simu Mkurugenzi Mtendaji Joseph Kusaga ananipigia simu kwa kitu nisichokielewa, Mkuu wa Mkoa ananipigia simu kunilaumu kuwa kuna kipindi nimekizuia, nikamwambia wewe tulia mimi nikampigia Mkuu wa Mkoa, ni kwa nini unakuja ofisini ukiwa na bunduki, akaniambia kwanini umesimamisha kipindi change, nikamwambia sio kipindi chako ni mimi ndio ninahusika,
Akasema kuna kipindi cha mwanamke aliyezaa na Gwajima, mbona hamjatumia, nikamwambia mimi siwezi kuruhusu kitu kama hicho, akakata simu,
zilizozagaa nchini kuwa studio za Radio Clouds na Clouds Tv zilivamiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akisindikizwa na askari wenye silaha.
Ukanda mfupi wa video, umesambazwa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya televisheni hapa nchini, ukimuonyesha Mkuu huyo wa Mkoa, akiwa na askari wenye silaha, akiingia kwenye ofisi inayodaiwa kuwa ndio ofisi za Clouds Mikocheni B, usiku wa Machi 17, 2017.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment