Friday, 10 March 2017

 RAIS wa Nigeria Muhammadu Buhari, (katikati), akipokewa na maafisa wa serikali yake kwenye uwanja wa ndege ya bkijeshi wa Kaduna Kaskazini mwa nchi hiyo Machi 9, 2017 baada ya kurejea akitokea nchini Uingereza ambako amekuwa huko kwa wiki kadhaa zilizoelezwa kuwa ni mapumziko ya kitabibu.
Rais Buhari akipiga picha na kiongozi wa kanisa la Anglicana Duniani, Justin Welby kabla ya kuondoka London


NA K-VIS BOLG/MASHIRIKA YA HABARI
RAIS wa Nigeria Muhammadu Buhari ameruhusiwa kutoka hospitali nchini Uingereza alikokuwa akipatiwa matibabu na sasa tayari amerejea nyumbani.
Taarifa za vyombo vya habari vya kimataifa zinasema, Rais Buhari mwenye umri wa mika 74, amewasili na ndege katika uwanja wa kijeshi kwenye mji wa Kaskazini wa Kaduna na sasa anajiandaa kwa safari ya kuelekea mji mkuu Abuja.
Kiongozi huyo wa Kijeshi wa zamani wa Nigeria, alikuwa nchini Uingereza tangu Januari 19, 2017 akiwa kwenye likizo ya matibabu nchini Uingereza.
Habari kuhusu nini hasa kinachomsumbua bado zinafanywa “siri”, na ndege iliyomchukua ililazimika kutua mjini Kaduna kwa vile uwanja wa Abuja umefungwa kwa muda wakati ukiendelea kufanyiwa ukarabati.
Taarisa rasmi ya serikali iliyotolewa jana Alhamisi Machi 9, 2017 imesema, Rais Buhari aliondoka Nigeria na kuelekea nchini Uingereza kwa “mapumziko” na alitumia mapumziko hayo kwa kufanyiwa uchunguzi wa kiafya.
“Mapumziko hayo yalirefushwa kutokana na ushauri wa madaktari wa kufanya vipimo zaidi na kumpa muda mpana wa mapumziko”. Taarifa hiyo ilisema.
“Hali ya kiafya ya Rais inatia shaka na sasa wakosoaji wanajiuliza kama Rais huyo yuko imara kuongoza Ofisi ya Rais.” Wakosoaji wanasema

Reactions:

0 comments:

Post a Comment