Tuesday, 28 March 2017


Mkazi wa mkoa wa Mara ambaye alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili ya matibabu ya upasuaji wa mgonjwa kufuatia majeraha ya kuunguzwa na maji ya moto kifuani, shingoni na mkononi,Bibi. Neema Mwita akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (hayupo pichani) kwa kitendo chake cha kumfariji na kumsaidia kupata matibabu ya hayo wakati akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.  Daktari bingwa wa Upasuaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dkt. Ibrahim Mkoma.
(PICHA NA FRANK SHIJA – MAELEZO).Daktari bingwa wa Upasuaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dkt. Ibrahim Mkoma akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu kuruhusiwa kwa mgonjwa aliyekuwa anapatiwa matibabu kutokana na majeraha ya kuunguzwa na maji ya moto kifuani, shingoni na mkononi, Bibi. Neema Mwita maarufu kama mgonjwa wa Magufuli. Neema alikuwa akipatiwa matibabu katika hospitali hiyo kufuatia msaada wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kuguswa na taarifa za mgonjwa huyo mapema mwezi wa pili mwaka huu hali iliyompelekea kuchukua jukumu la kumsaidia.Mkuu wa Jengo la Sewahaji Bibi. Salome Mayenga (kushoto) na Mkuu wa Wodi namba 24 Sewahaji, Muhimbili Bibi. Georgina Kabaitileki.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment