Wednesday, 15 March 2017


RAIS John Pombe Magufuli, ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, (Bunge), Bw. Uledi Abass Mussa kuanzia leo Machi 15, 2017.
Taarifa ya Ikulu iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa ikimnukuu Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imesema, sambamba na hatua hiyo Katibu Mkuu Uledi pia amesimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake.
Taarifa hiyo imezitaja tuhuma hizo kuwa ni kushindwa kwa Bw. Uledi kusimamia taratibu zinazotakiwa katika kushughulikia taratibu za uwekezaji.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment