Monday, 20 March 2017

Rais John Pombe Magufuli, akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul makonda, leo Machi 20, 2017 baada ya kutoa hotuba ya ukaribisho kwenye hafla ya uwekaji jiwe la msingi ujenzi wa Flyover Ubungo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Rais wa Benki ya Dunia, Dkt. Jim Yong Kim.
NA K-VIS BLOG
RAIS John Pombe Magufuli, amemtetea Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kupuuza tuhuma mbalimbali zinazoendelea kutolewa dhidi ya Mkuu huyo wa Mkoa.
Akizunguzma kwenye hafla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara za juu kwenye makutano ya barabara za Mandela, Morogoro na Sam Nujoma jijini Dar es Salaam leo Machi 20, 2017, almaarufu kama Flyover, Rais Magufuli alisema. “Wana Dar es Salaam tunatumia muda mwingi kwenye umbea, tunapoteza muda mwingi kujadili personalities, niwaombe Wana-Dar es salaam tuache kupoteza muda tuchape kazi,  Mimi huwa sionyeshwi njia tayari nimekwishaonyeshwa njia na chama change cha CCM kupitia Ilani ya uchaguzi, swala la kuandikwa kwenye mitandao siyo tija kwangu.” Alisema.
Akifafanua zaidi Rais Magufuli alsiema, yeye hatulazimishwa na mtu kufanya uamuzi Fulani kwani anajiamini, “Makonda wewe chapa kazi, suala la kuandikwa kwenye mitandao si tija kwangu wewe chapa kazi.” Alisisitiza Rais Magufuli.
Kauli ya Rais Magufuli inakuja muda mfupi baada ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nanuye akiuunda kamati ya watu watano kuchunguza ni kwanini Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, “alivamia” studio za televisheni ya Clouds akiwa na askari wenye bunduki usiku wa saa 4:45 Ijumaa iliyopita.
Akizungumza wakati alipotembelea ofisi za Clouds Media Group, (CMG), huko Mikocheni B jijini Dar es Salaam leo Machi 20, 2017, waziri Nape alisema, kamati hiyo itafanya uchunguzi kwa masaa 24 na kuwasilisha ripoti kwake. "Kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makodna, cha kuingia kwenye studio hizo akiwa na askari wenye silaha ni kuinajisi tasnia ya habari" Alisema Nape.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, anatuhumiwa kuingia kwa nguvu kwenye studio za Clouds akiwa na askari wenye bunduki kwa nia ya kushinikiza ni kwanini habari ya mama aliyefanyiwa mahojiano na watangazaji wa kipindi cha DE Weekend Chat Shaw, (SHILAWADU), kuwa alizaa na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Dkt. Josephat Gwajima.
Hata hivyo baada ya tathmini ya kitaalamu iliyofanywa ilionekana taarifa hiyo isipeperushwe hewani kwani anayetuhumiwa hakupatikana ili nay eye aeleze upande wake.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment