Monday, 13 March 2017RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amekutana na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein, Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo Machi 13, 2017.
Taarifa fupi ya Ikulu iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari imesema, marais hao wawili walizungumzia masuala mbalimbali ya husuyo kazi kubwa waliyonayo ya kuongoza nchi.
Aidha taarifa hiyo iliyosainiwa na Naibu Mkurugenzi wa Kurugenziya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Jaffer Haniu, imesema, Rais Magufuli amemtakia heri ya siku ya kuzaliwa ya Dkt. Shein ambayo ameiadhimisha leo Machi 13, 2017
Pichani 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein walipokutana kwa mazungumzo Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Jumatatu Machi 13, 2017.(PICHA NA IKULU)
Reactions:

0 comments:

Post a Comment